Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo afichua alivyokaribia kustaafu

RONALDO Pict

Muktasari:

  • Ronaldo, 41, hakutoa uhakika kuhusu hatma yake na Ureno baada ya kushiriki Kombe lake la Dunia kwa mara ya tano, ambako Ureno ilitolewa katika hatua ya 16 bora kwa kufungwa bao 1-0 na Hispania, ambao baadaye walitwaa ubingwa.

LISBON, URENO: CRISTIANO Ronaldo amefichua kuwa aliwahi kufikiria kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Ureno baada ya Kombe la Dunia, lakini ameamua kuendelea kuitumikia nchi yake akiamini bado ana mchango mkubwa wa kutoa.

Ronaldo, 41, hakutoa uhakika kuhusu hatma yake na Ureno baada ya kushiriki Kombe lake la Dunia kwa mara ya tano, ambako Ureno ilitolewa katika hatua ya 16 bora kwa kufungwa bao 1-0 na Hispania, ambao baadaye walitwaa ubingwa.

Hata hivyo, licha ya matarajio kwamba angeaga soka la kimataifa, Ronaldo alijumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha wachezaji 25 cha kocha mpya Jorge Jesus kwa ajili ya mechi za Nations League dhidi ya Wales, Denmark na Norway.

Akizungumza kabla ya mchezo wao dhidi ya Wales, Ronaldo alikiri kuwa alifikiria kuachana na timu hiyo, lakini akaamua kuendelea.

“Ndiyo, huwa nafikiria maamuzi yangu. Nafikiria kila kitu. Unaniona hapa, hivyo nimeamua kuendelea,” amesema Ronaldo.

RONA 03

Mshambuliaji huyo wa Al-Nassr amesema bado anaamini ana uwezo wa kusaidia Ureno kufikia malengo yake, si kwa kufunga mabao pekee bali pia kwa kuwaongoza wachezaji wengine nje ya uwanja.

“Bado naamini ninaweza kuisaidia timu ya taifa kufikia kile inachotaka. Naweza kutoa msaada wangu, si kwa mabao tu, bali pia nje ya uwanja,” amesema.

Ronaldo amesisitiza kuwa kizazi kipya cha wachezaji kinaendelea kuibuka, lakini yeye bado anataka kuhakikisha anafanya kazi yake uwanjani kwa kufunga na kusaidia timu kushinda.

“Wakati watakaposema hawanihitaji tena kwenye timu ya taifa, nitakuwa mtu wa kwanza kuondoka. Nitakapohisi siongezi chochote kwenye timu au ninaharibu mazingira, nitakuwa wa kwanza kuondoka. Nitachukua mzigo wangu na kuondoka,” amesema.

RONA 02

Ronaldo pia amesema takwimu zake zinaonyesha bado ana mchango kwa Ureno, huku akiahidi kuwa hata baada ya kuondoka ataendelea kuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo.

“Wareno bado wananihitaji, ndiyo maana bado niko hapa. Angalia tu takwimu, unaweza kufanya hesabu zako. Bado nafanya vizuri. Siku ambayo hawatanihitaji, hakuna tatizo, nitaondoka. Nitakuwa shabiki namba moja wa shirikisho hili,” amesema.


RONA 04

HAJUI ATAFIKA 2028?

Ronaldo pia aliulizwa kama ataendelea kuichezea Ureno hadi fainali za Nations League msimu ujao au hadi Euro 2028, lakini hakutoa jibu la moja kwa moja.

Badala yake, amesema kwa sasa anataka kuishi katika wakati uliopo na kuendelea kufanya kile anachoweza kudhibiti.

Akizungumzia wakosoaji wake, Ronaldo amesema baadhi ya vyombo vya televisheni vimekuwa vikimkosoa vikali, lakini ameshazoea hali hiyo baada ya kuwa kwenye soka la kiwango cha juu kwa zaidi ya miaka 20.

“Siwezi kuwa mkweli kwa asilimia 100 kila wakati, wakati mwingine lazima niwe wa kisiasa,” amesema.

“Naelewa baadhi ya vituo vya televisheni vinapenda kunikosoa. Wamejaribu kuniua kwa bunduki, lakini bado ninaweza kujiepusha nayo. Nimezoea. Nimekuwa nikifanya hivi kwa zaidi ya miaka 20.”

Ronaldo ameongeza: “Kile ninachoweza kukidhibiti, nitakidhibiti. Kile nisichoweza kukidhibiti, sitakihangaikia.”


RONA 01

MABAO 1,000 YANAKUJA

Mshambuliaji huyo pia alizungumzia ndoto yake ya kufikisha mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.

Ronaldo, ambaye hadi sasa amefunga mabao 979, amebakiza mabao 21 tu kufikisha rekodi hiyo, lakini amesema hataki kujipa presha kubwa kuhusu hilo.

“Itakuwa kama sherehe kufunga bao langu la 1,000 nikiwa na timu ya taifa. Itakuwa kilele cha hadithi nzuri,” amesema.

“Nimesema nataka kufikia lengo hilo na nitalifikia, lakini sina presha nalo.”


RONA 05

JESUS: RONALDO NI ALAMA YA URENO

Kocha mpya wa Ureno, Jorge Jesus, tayari amethibitisha kuwa Ronaldo ataanza katika mchezo dhidi ya Wales.

Jesus amemtaja Ronaldo kama “alama ya Ureno”, akionyesha imani yake kwa nahodha huyo mkongwe ambaye amecheza mechi 233 kwa timu ya taifa na kufunga mabao 146.

Kwa sasa Ronaldo ameendelea kuwepo kwenye kikosi cha Ureno licha ya maswali mengi kuhusu hatma yake ya kimataifa, huku mwenyewe akisisitiza kuwa bado yuko tayari kuitumikia nchi yake kwa muda ambao timu itamhitaji.