Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchezaji ang’oolewa meno matatu, mechi yavunjika

Muktasari:

  • Tukio hilo lilitokea baada ya kipindi cha kwanza, ambapo hali iligeuka kuwa mbaya baada ya Dumay, mwenye umri wa miaka 25, kudaiwa kushambuliwa na mmoja wa watu waliokuwa kwenye benchi la GVVV.

AMSTERDAM, Uholanzi: MCHEZO wa Ligi Daraja la Tatu nchini Uholanzi kati ya IJsselmeervogels na GVVV ulisitishwa baada ya mchezaji Quiermo Dumay kupoteza meno matatu kufuatia vurugu zilizozuka kwenye handaki la kuingilia vyumba vya kubadilishia nguo.

Tukio hilo lilitokea baada ya kipindi cha kwanza, ambapo hali iligeuka kuwa mbaya baada ya Dumay, mwenye umri wa miaka 25, kudaiwa kushambuliwa na mmoja wa watu waliokuwa kwenye benchi la GVVV.

Vurugu hizo zilihusisha wachezaji na mashabiki wa pande zote mbili, hali iliyolazimisha polisi kuingilia kati na kuzunguka eneo la handaki ili kuzuia watu wengine kuingia. Dumay alibaki akiwa amejeruhiwa, huku akiwa amepoteza meno matatu na jezi yake ikiwa imejaa damu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Uholanzi, wachezaji wa IJsselmeervogels walikataa kurejea uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili, huku klabu hiyo ikitarajiwa kutoa taarifa rasmi kwa polisi kuhusu tukio hilo. Polisi walilazimika kudhibiti njia za kuingia kwenye handaki hilo, huku mashabiki nao wakitolewa uwanjani mjini Bunschoten kutokana na hofu ya uwezekano wa kutokea kwa vurugu zaidi baada ya mchezo.

Maafisa walieleza kuwa tayari kulikuwa na makabiliano kati ya mashabiki kwenye jukwaa kabla ya tukio kubwa lililotokea kwenye handaki.

Wakati mchezo ukisitishwa, GVVV ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Katibu wa GVVV alisema klabu hiyo ilishtushwa na tukio hilo na kwamba linahitaji uchunguzi wa kina.

“Kilichotokea mchana huu ni jambo la kusikitisha, na kusema hivyo ni kupunguza uzito wa tukio. Ni jambo la kushangaza na ambalo halijawahi kutokea.

“Tunapaswa kulichunguza kwa kina. Ninachoelewa ni kwamba chanzo kilikuwa msaidizi wa kocha wa GVVV kumpiga mmoja wa wachezaji wao, ambaye alianguka na kubaki chini kwa muda.”

Hayo ndiyo niliyoelezwa. Baada ya hapo hali ilizidi kuwa mbaya kwa sababu mchezaji anapigwa, anaanguka chini akiwa anatokwa damu na meno yakimtoka kwenye handaki, hilo linaweza kusababisha matatizo makubwa. “Wafanyakazi waliomba msaada kwa ajili ya mchezaji wetu pamoja na yule aliyefanya shambulio hilo. “Sijui sababu ya tukio hilo ilikuwa nini. Ninachojua ni kwamba mchezaji alipigwa, akaanguka chini, meno yakamtoka na kuanza kutokwa damu. “Baada ya hapo unaona hali ikizidi kuwa mbaya kwa sababu tukio lenyewe lilikuwa la kutisha na lilikuwa na msisimko.”

Mchezo huo haukuendelea baada ya mapumziko, huku mamlaka husika zikitarajiwa kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha vurugu hizo na hatua za kuchukua.