Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matajiri Saudi Arabia waweka noti kwa Kane

HARRY KANE Pict

Muktasari:

  • Inadaiwa katika mkataba wake kuna kipengele ambacho kinampa nafasi ya kuondoka kwa timu inayomhitaji kulipa kiasi kisichozidi Pauni 60 milioni, lakini kipengele hicho kitafanya kazi mwisho wa msimu huu na Kane mwenyewe atatakiwa kusema kwamba anataka kuondoka ifikapo Januari.

RIYADH, SAUDI ARABIA: MATAJIRI wa Saudi Arabia kutoka timu ya Al-Hilal, wapo tayari kumpa Harry Kane  pesa ndefu inayofikia Pauni 261 milioni kama mshahara wa kuwatumikia kwa miaka mitatu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bild, nyota huyo wa Bayern Munich ambaye amekuwa katika kiwango cha juu kabisa katika miezi miwili ya mwanzo wa msimu wa 2025-26, akivunja rekodi kadhaa, mustakabali wake kuelekea mwisho wa msimu huu bado ni kizungumkuti.

Inadaiwa katika mkataba wake kuna kipengele ambacho kinampa nafasi ya kuondoka kwa timu inayomhitaji kulipa kiasi kisichozidi Pauni 60 milioni, lakini kipengele hicho kitafanya kazi mwisho wa msimu huu na Kane mwenyewe atatakiwa kusema kwamba anataka kuondoka ifikapo Januari.

Tovuti ya Sport BILD,  imefichua kuwa mabingwa wa Saudi Al-Hilal wako tayari kutoa ofa ya mshahara wa Pauni 87 milioni kwa mwaka ambao utamfanya kuwa mchezaji wa pili kuwahi kupokea mshahara mkubwa katika historia ya timu hiyo baada ya Neymar.

Chanzo kilichotoa taarifa hiyo kilisema: ”Wamekuwa wakimtaka  kwa muda. Walimtaka hata wakati ule hajajiunga rasmi na Bayern . Walitaka kuingilia dili katikati, lakini Bayern tayari walikuwa wameshafikia makubaliano.”

Kushinda mataji ilikuwa ni sababu kubwa iliyosababisha Kane kuondoka Spurs na kujiunga na Bayern katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2023.

Hata hivyo, katika msimu wake wa kwanza hakufanikisha hilo na badala yake akafanikiwa msimu uliopita ambapo alishinda taji lake la kwanza la Ligi Kuu.