Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United kunufaika na adhabu ya City, AI yataja watano

Muktasari:

  • Utabiri uliofanywa na akili unde (AI) unaonyesha Man United inaweza kumnasa hadi wachezaji watano wa City iwapo rufaa ya miamba hiyo itashindwa na adhabu kali, ikiwamo kushushwa daraja, itatekelezwa.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United inaweza kuwa miongoni mwa klabu zitakazonufaika zaidi endapo Manchester City itashushwa daraja kutokana na sakata lake la ukiukaji wa kanuni za kifedha za Ligi Kuu England.

Utabiri uliofanywa na akili unde (AI) unaonyesha Man United inaweza kumnasa hadi wachezaji watano wa City iwapo rufaa ya miamba hiyo itashindwa na adhabu kali, ikiwamo kushushwa daraja, itatekelezwa.

City imepatikana na hatia ya makosa yote yanayohusiana na tuhuma za ukiukaji mkubwa wa kanuni za kifedha katika kipindi cha misimu tisa, pamoja na makosa mengi ya kushindwa kushirikiana kikamilifu na uchunguzi wa Ligi Kuu.

Hata hivyo, City imeendelea kukana makosa hayo na kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Iwapo rufaa hiyo itakataliwa, klabu hiyo inaweza kukabiliwa na adhabu mbalimbali, zikiwamo kupokonywa pointi, faini na hata kushushwa daraja.

Kwa mujibu wa utabiri huo wa AI, Real Madrid ndiyo inaweza kunufaika zaidi, ikitajwa kuwa na nafasi ya kuwasajili hadi nyota wanane wa City, akiwamo mshambuliaji Erling Haaland.

Haaland, ambaye amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na Real Madrid, anaweza kuungana na Enzo Fernandez, Phil Foden, Ayyoub Bouaddi, Abdukodir Khusanov, Vitor Reis, Josko Gvardiol na Mateo Kovacic.

United, kwa upande wake, imetajwa kuwa inaweza kuwasajili Gianluigi Donnarumma, Elliot Anderson, Matheus Nunes, Nico O’Reilly na Rico Lewis.

Liverpool nayo inaweza kunufaika kwa kuwasajili Antoine Semenyo, Marc Guehi, Rayan Ait-Nouri na nahodha wa City, Ruben Dias.

Arsenal imepewa nafasi ya kumnasa Jeremy Doku, wakati Chelsea inaweza kumrudisha Marcus Bettinelli.

Kwa upande mwingine, Paris Saint-Germain imetajwa kuwa inaweza kumrudisha Rayan Cherki nchini Ufaransa, huku Iliman Ndiaye akitabiriwa kurejea Everton.

Mateo Kovacic ametajwa kurejea Real Madrid, wakati Geronimo Rulli na Allan wanaweza kujiunga tena na Real Sociedad na Palmeiras, mtawalia.

Hata hivyo, haya ni makadirio ya AI tu, si mpango rasmi wa usajili wa klabu hizo wala uthibitisho kwamba wachezaji hao wataondoka City.