Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City yakomaa na Anderson

FIFA Pict

Muktasari:

  • Wiki iliyopita iliripotiwa Anderson, 23, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa England, anaipenda zaidi Manchester City kuliko Manchester United kama ataondoka Forest.

LONDON ENGLAND: Manchester City imekataliwa ofa yao ya kwanza waliyopeleka kwa ajili ya kumsajili kiungo Elliot Anderson kutoka Nottingham Forest.

Wiki iliyopita iliripotiwa Anderson, 23, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa England, anaipenda zaidi Manchester City kuliko Manchester United kama ataondoka Forest.

Kwa sasa kuna matarajio Anderson ataondoka uwanja wa City Ground msimu huu na City wameonyesha nia yao kwa kuwasilisha ofa ya kwanza ambayo imekataliwa na Forest.

Anderson alikuwa na msimu bora Nottingham Forest na amejumuishwa katika kikosi cha England kinachoongozwa na kocha Thomas Tuchel kwa ajili ya Kombe la Dunia.

Iwapo uhamisho huo utatimia, ada yake inaweza kuweka rekodi mpya kwa mchezaji wa Uingereza na kuzidi pauni105 milioni ambazo Arsenal walilipa West Ham United mwaka 2023 ili kumsajili Declan Rice.

Manchester City wamekuwa wakimfuatilia Anderson kwa muda mrefu tangu alipokuwa akitokea akademi ya Newcastle United. Kwa sasa mchezaji huyo yuko katika maandalizi ya Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani, Canada na Mexico, lakini mazungumzo kati ya klabu hizo yanaweza kuendelea.

Baada ya nahodha Bernardo Silva kuondoka, City wanatafuta kuimarisha safu yao ya kiungo na Anderson amewekwa juu ya orodha ya wachezaji wanaowahitaji.

Kiungo wa Newcastle, Sandro Tonali, pia anaripotiwa ni miongoni mwa wanaothaminiwa na City. Taarifa zinaeleza mchezaji huyo wa Italia amekuwa akifuatiliwa kwa muda mrefu kama lengo la baadaye la klabu hiyo.

Wakati huo huo, Nico Gonzalez, ambaye hakupata nafasi katika kikosi cha Hispania cha Kombe la Dunia, pia alipoteza nafasi yake chini ya kocha Pep Guardiola msimu uliopita, anaweza kuondoka ikiwa ofa nzuri itawasilishwa.