Man City mambo bado ni magumu EPL
Muktasari:
- Wageni Fulham ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika mechi hiyo kupitia kwa Rodrigo Muniz katika dakika ya 16.
MANCHESTER, ENGLAND: Manchester City imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Fulham nyumbani kwenye Uwanja wa Etihad leo Jumamosi, Novemba 21, 2026 matokeo yanayozidi kuipunguza kasi katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
Wageni Fulham ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika mechi hiyo kupitia kwa Rodrigo Muniz katika dakika ya 16.
Man City walisawazisha bao hilo katika dakika ya 57 kupitia kwa Elliot Anderson.
Sare hiyo imeifanya Man City kuendelea kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England (EPL) ikifikisha pointi 22.
Kwa upande wa Fulham, matokeo hayo yameifanya ifikishe pointi 11 na kusogea kwa muda hadi katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi.
Huo ni mchezo wa nne ,mfululizo kwa Man City kutopata ushindi kwenye EPL tangu imara ya mwisho ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ipswich Town, Oktoba 17, 2026.
Baada ya mechi ya leo, kibarua kinachofuata cha Man City ni dhidi ya Napoli kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumanne, Novemba 24 mwaka huu.
Mchezo unaofuata wa Fulham ni dhidi ya Bournemouth, Novemba 29, 2026.