Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baraka nyingi Rodrygo akiwa na Gabriella!

Muktasari:

  • Rodrygo ambaye alithitisha uhusiano wake na Gabriella Septemba, Machi alifanyiwa upasuaji na sasa ameanza mazoezi mapesi huku akitarijiwa kurejea tena uwanjani Desemba au mapema mwakani.

WAKATI mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo Goes akiendelea kuuguza majeraha, hivi karibuni mpenzi wake kutokea kwao Brazil, Gabriella Lenzi alieleza jinsi alivyo na matumaini makubwa kwa mchezaji huyo akiamini atarejea uwanjani na kuandika historia yake.

Rodrygo ambaye alithitisha uhusiano wake na Gabriella Septemba, Machi alifanyiwa upasuaji na sasa ameanza mazoezi mapesi huku akitarijiwa kurejea tena uwanjani Desemba au mapema mwakani.

“Natamani ungeweza kujitazama kupitia macho yangu katika kipindi hiki cha safari yako. Labda ungeelewa ukubwa wa jinsi ninavyojivunia wewe. Maendeleo yako, uimara wako na namna ambavyo hukati tamaa hata katika siku ngumu zaidi, vinanifanya nizidi kukuheshimu na kuvutiwa na wewe.

“Nina bahati ya kushuhudia safari yako ya kujijenga upya inayostaajabisha kama mafanikio yote ambayo umewahi kuyapata ndani ya uwanja. Nina hamu kubwa ya kukuona ukifanya tena kile ambacho ulizaliwa kukifanya.

“Lakini ushindi mkubwa zaidi katika maisha yako ya soka unaupata sasa na unaishi bila mashabiki wa kukushangilia, bila kuwepo uwanjani na bila kusikia makofi ya watu.

“Mungu yupo katika kila hatua ya safari hii na yale ambayo amekuandalia ni makubwa zaidi ya tunavyoweza kuyawaza. Sehemu nzuri zaidi ya historia yako bado haijaandikwa,” alieleza Gabriella katika Instagram.

Rodrygo alijibu ujumbe huo kwa kuandika; Asante mpenzi wangu kwa kuniunga mkono katika kila hali, hasa katika nyakati hizi ngumu zaidi, lakini ambazo tuna uhakika yaliyo bora kutoka kwa Mungu yanakaribia kutimia... Nakupenda sana kipenzi changu!.

Mnamo Septemba, ndipo Rodrygo alithibitisha hadharani katika uhusiano wa kimapenzi na Gabriella ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuhusishwa na staa wa soka, Neymar Jr, pamoja na mwanamuziki Justin Bieber.

Rodrygo alitangaza uhusiano huo kupitia ujumbe wa kimahaba aliouandika kwenye mitandao ya kijamii na siku hiyo pia Gabriella alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Katika Insta Stories, Rodrygo aliposti picha akiwa pamoja na Gabriella na kuambatanisha na ujumbe uliosomeka: ‘Heri ya siku ya kuzaliwa, mrembo wangu. Nakupenda.’

Tetesi za uhusiano wa wawili hao zilikuwepo tangu mwaka 2025 lakini aliamua kukaa kimya bila kujibu wala kuelezea chochote kile. Oktoba mwaka huo, walivutia hisia za wengi baada ya kuhudhuria sherehe za Halloween zilizoandaliwa na Vini Jr. na Virginia Fonseca jijini Madrid.

Miezi kadhaa baadaye, wawili hao walionekana tena pamoja hadharani. Julai mwaka huu, walipigwa picha wakiwa pamoja katika mazoezi ya mashindano ya magari ya Formula 1 jijini Madrid. Picha hizo zilichapishwa na jarida la Ufaransa la Paris Match, kitu kilichokoleza tetesi za uhusiano wao.

Mwaka 2014, Gabriella alitajwa na gazeti la Hispania la AS huenda alikuwa na uhusiano na Neymar wakati huo, gazeti hilo liliripoti kuhusu madai ya uhusiano wao, ambao hata hivyo haukuwahi kuthibitishwa na upande wowote.

Baada ya taarifa hizo kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, Gabriella alianza kupokea jumbe nyingi kutoka kwa mashabiki ambao walitamani kujua ukweli wa jambo hilo.

Mwaka 2017, Gabriella alitajwa tena kwenye vyombo vya habari baada ya mwanamuziki Justin Bieber kutembelea Jiji la Rio de Janeiro, Brazil.

Kwa mujibu wa gazeti la Extra, inadaiwa Bieber alivutiwa na mwanamitindo huyo wakati wa sherehe iliyofanyika kwenye hoteli ya kifahari ya Fasano, ikiwa ni muda mfupi baada ya mwanamuziki huyo kufanya show katika uwanja wa Praca da Apoteose.

Gazeti hilo liliripoti Bieber alijaribu kumkaribia Gabriella, lakini mrembo huyo inadaiwa hakuwa tayari kuwa na ukaribu na msanii huyo wa Canada. Hata hivyo, ilielezwa baadaye Bieber aliondoka katika sherehe hiyo akiwa ameongozana na wanawake wengine waliohudhuria sherehe hiyo.

Lakini baada ya kuthibitishwa uhusiano wake na Rodrygo, sasa Gabriella anaingia katika kundi la warembo wanaotoka mastaa wa soka Ulaya, huku akiendelea kujijengea umaarufu kwao Brazil akiongeza idadi ya mastaa wa nchi hiyo wanaoishi jijini Madrid, Hispania.

Lakini Gabriella ni nani hasa?, mrembo huyu ni mshawishi wa mitandao ya kijamii (influence) akiwa na wafuasi (followers) zaidi ya milioni 1.4 Instagram na huposti maudhui kuhusu safari zake pamoja na matangazo ya bidhaa za vinywaji na vyakula vya kuongeza nguvu, pamoja na mavazi.

Gabriella anatokea Jaragua do Sul, jimbo la Santa Catarina nchini Brazil, ni binti wa Alessander Lenzi, anayetambulika kama mmoja wa watu wakubwa katika mchezo wa mashindano ya pikipiki za majini (Jet Ski) nchini Brazil.

Pia Gabriella aliwahi kujihusisha na mchezo huo na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Brazil katika mashindano ya ngazi ya wachezaji wasio rasmi. Historia ya familia yake katika mchezo huo imemfanya aendelee kuwa karibu na ulimwengu wa mashindano hayo.