Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamelodi Sundowns yaichapa Orlando Pirates yatwaa taji

SAUZ Pict

Muktasari:

  • Mabao ya Teboho Mokoena katika kipindi cha kwanza na mshambuliaji wa akiba, Iqraam Rayners, kipindi cha pili yaliihakikishia Sundowns ushindi dhidi ya Pirates, iliyokuwa ikitetea ubingwa huo baada ya kuutwaa kwa misimu minne mfululizo.

PRETORIA, AFRIKA KUSINI: KOCHA wa Mamelodi Sundowns, Miguel Cardoso ameelezea furaha yake baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la MTN8 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Orlando Pirates.

Mabao ya Teboho Mokoena katika kipindi cha kwanza na mshambuliaji wa akiba, Iqraam Rayners, kipindi cha pili yaliihakikishia Sundowns ushindi dhidi ya Pirates, iliyokuwa ikitetea ubingwa huo baada ya kuutwaa kwa misimu minne mfululizo.

Kwa Sundowns, mabingwa hao wa Afrika, ushindi huo ulikuwa muhimu baada ya miaka kadhaa ya kukosa taji hilo. Huo ni ubingwa wao wa tano wa MTN8 na wa kwanza tangu walipoutwaa mwaka 2021.

SAU 01

Akizungumza na SuperSport TV baada ya mchezo, Cardoso amesema ushindi huo umetokana na moyo wa kupambana, ari, nidhamu ya kimchezo na mshikamano wa kikosi chake.

“Kwa moyo, ari, mpangilio na upendo mkubwa. Ni vigumu sana kucheza dhidi ya Orlando Pirates, na ni vigumu zaidi kushinda kwa tofauti ya mabao mawili bila kuruhusu bao,” amesema Cardoso.

Kocha huyo amesema furaha yake kubwa ilikuwa kuwapa mashabiki wa Sundowns taji la ndani, akiwapongeza kwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.

SAU 02

“Taji hili ni kwa ajili ya watu hawa. Wanastahili, wamejitokeza kwa wingi, na ninaamini ulikuwa wakati wa kuwapa kombe la ndani.

“Ni jambo gumu, lakini wakati mwingine watu hawaelewi kwamba ni lazima kuweka vipaumbele kati ya mashindano. Kufanya hivyo pia kunatumia nguvu za wachezaji,” ameongeza.

Cardoso amesema tangu alipojiunga na klabu hiyo, aliweka wazi kuwa kutwaa taji hilo ni miongoni mwa malengo yake, huku akisisitiza kuwa wachezaji wamefanya kazi kubwa kufanikisha ushindi huo.

SAU 03

Alikiri kuwa ratiba ya mashindano mbalimbali itakuwa changamoto kwa Sundowns, hasa wanapolazimika kucheza mechi za ligi na mashindano ya kimataifa kwa vipindi vifupi.

“Ni wazi tulitaka kuipa klabu hii kombe. Wachezaji wamefanya kazi kwa bidii sana, na tangu siku yangu ya kwanza nilisema hili linapaswa kuwa lengo letu.

“Hatuna uhakika wa nini kitakachofuata kwa sababu tutashiriki mashindano mengi. Itakuwa vigumu kucheza dhidi ya Carling katikati ya wiki wakati tunakuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki.

“Lakini hawa wachezaji wanaelewana na wanaaminiana. Wanatuamini sisi, nasi tunawaamini wao. Hongereni kwa mchezo mzuri sana. Tulielewa namna ya kucheza mchezo huu. Jambo si namna unavyocheza pekee, bali pia namna unavyopambana. Tulikuwa jasiri na tulifanya vizuri sana,” amesema Cardoso.