Makocha wengine wanaomfuata Sage
Muktasari:
- Viongozi wa klabu za ligi hiyo wameonyesha uvumilivu katika miezi ya mwanzo ya msimu, na hii huenda ni kutokana na sababu kadhaa, miongoni mwazo ni kuchelewa kidogo kwa kuanza kwa ligi kutokana na fainali za Kombe la Dunia, pamoja na klabu tisa kubadilisha makocha katika kipindi cha mapumziko ya majira ya joto.
KATIKA misimu 13 iliyopita, mara nyingi kocha wa kwanza wa Ligi Kuu England amekuwa akitimuliwa kabla ya Novemba. Hivyo, michezo ya wikiendi ya kwanza mwezi huu ilikuwa muhimu kwa makocha kadhaa wanaokabiliwa na presha mmoja tayari keshaondoka.
Viongozi wa klabu za ligi hiyo wameonyesha uvumilivu katika miezi ya mwanzo ya msimu, na hii huenda ni kutokana na sababu kadhaa, miongoni mwazo ni kuchelewa kidogo kwa kuanza kwa ligi kutokana na fainali za Kombe la Dunia, pamoja na klabu tisa kubadilisha makocha katika kipindi cha mapumziko ya majira ya joto.
Hata hivyo, siyo jambo la kawaida katika miaka ya karibuni kwa klabu zote kuendelea na makocha wao hadi Novemba. Ni makocha gani wanaomfuata Pierre Sage wa Crystal Palace aliyefukuzwa jana?
Palace wako mkiano mwa msimamo baada ya kupoteza mechi nne zilizopita. Wameruhusu mabao 24, ambayo ni sita zaidi ya timu nyingine yoyote. Pia, wamewaruhusu wapinzani kupiga mashuti 88 zaidi ya yale waliyopiga wao wenyewe msimu huu, tofauti kubwa zaidi katika ligi. Sage aliteuliwa mwanzoni mwa msimu, lakini muda wake unaanza kuyoyoma.
MAKOCHA WANNE KWENYE SHIDA
Michael Carrick anaonekana kuwa kocha mwenye uwezekano mkubwa wa kutimuliwa wakati wowote, hasa baada ya Manchester United kufungwa mabao 3-0 nyumbani na Bournemouth wiki kadhaa zilizopita. Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo uliamua kutomtimua mapema. Inawezekana msimamo wa mashabiki uliathiri uamuzi huo. Licha ya kipigo, mashabiki waliendelea kumuunga mkono Carrick, huku wachezaji, wamiliki wa klabu na mkurugenzi wa ufundi wakizomewa. Ilikuwa wazi kuwa kocha huyo bado alikuwa na uungwaji mkono wa mashabiki.
Baadaye, United walifungwa mabao 2-0 na Chelsea, matokeo ambayo kwa kiasi fulani yalichangiwa na kadi nyekundu aliyoonyeshwa Lisandro Martínez. Hata hivyo, siku chache baadaye timu ilionyesha uwezo wa kurejea mchezoni baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 na kuifunga Roma katika Ligi ya Mabingwa Ulaya 3-2.
Inawezekana United walimpa Carrick muda zaidi ili kuandaa mpango wa kumpata mrithi wake, ambao unaweza kutekelezwa, hasa ikizingatiwa kuwa wanapitia mwanzo mbaya zaidi wa msimu katika ligi ya daraja la juu kwa miaka 40.
Oliver Glasner, ambaye Pierre Sage alichukua nafasi yake, naye anapitia kipindi kigumu akiwa Nottingham Forest. Baada ya mechi 10, Forest wanashika nafasi ya 16 wakiwa na pointi tisa. Hata hivyo, takwimu zinaweza kuwashawishi viongozi wa klabu hiyo kumpa muda zaidi, kwani wako nafasi ya tatu wakiwa na pointi 15.5 za mabao yanayotarajiwa, jambo linaloashiria kuwa wamekuwa na bahati mbaya katika matokeo yao.
Sehemu ya tatizo ni kushindwa kutumia nafasi za kufunga mabao. Forest wamefunga mabao machache kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na yanayotarajiwa kuliko timu nyingine yoyote msimu huu (-8.3). Hata hivyo, kipigo cha mabao 3-1 walichoipa Manchester City kinampa kocha huyo nafasi ya kupumua kwa sasa.
Sunderland wanafuata katika orodha ya timu zilizoshindwa kufikia matarajio ya mabao ya kufunga wakiwa na -6.2, hali inayomuweka kocha Régis Le Bris kwenye presha. Le Bris aliiongoza timu hiyo kupanda daraja 2025 na kumaliza katika nafasi ya saba msimu uliopita, hivyo anaweza kuwa amejijengea nafasi ya kupewa muda zaidi. Hata hivyo, uvumilivu unaonekana kuanza kuisha. Hata wikiendi iliyopita Sunderland waliichapa Chelsea kwa bao 1-0.
Nayo Coventry City iliyopo nafasi ya 17 juu ya Manchester United kocha wake, Frank Lampard yupo kwenye mtihani akikabiliwa na wakati mgumu zaidi ikizngatiwa kwamba mwishoni mwa wiki iliyopita alipoteza kwa mabao 3-1 mbele ya Everton.
MIEZI YA MABADILIKO
Klabu za Ligi Kuu England zimekuwa na uvumilivu hadi sasa, lakini je, ni subira au hofu inayozifanya zisiwachukulie hatua makocha waohao wanne? Historia inaonyesha kuwa Novemba na Desemba ndiyo miezi inayoongoza kwa mabadiliko ya makocha katikati ya msimu. Kila mmoja umeshuhudia makocha 35 wakiondoka tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu England 1992/93. Hivyo, ligi inakaribia kipindi ambacho mabadiliko ya benchi la ufundi huwa mengi zaidi.
Kwa kuzingatia hilo na ukweli kwamba makocha kadhaa wanahangaika karibu na mkiani mwa msimamo, kuondoka kwa mmoja kunaweza kusababisha wengine kufuata. Matumaini ya kupata kile kinachoitwa ‘msisimko wa kocha mpya’ ni kishawishi kikubwa kwa klabu, hasa katika hatua hii ya msimu ambayo ushindi wa mechi chache unaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa hali ya timu. Klabu moja ikiamua kumtimua kocha wake, nyingine zinaweza kufuata kwa hofu ya kuchelewa kuchukua hatua.
Pia kuna mambo mengine ya kuzingatia msimu huu. Hakuna timu iliyopanda daraja inayopitia matatizo makubwa sana, jambo ambalo siyo la kawaida. Vilevile, hakuna timu iliyojitenga kwa kiwango cha kutia wasiwasi mkiani mwa ligi, kama ilivyokuwa kwa Wolves msimu uliopita.
Dalili za awali zinaonyesha kuwa kutakuwa na ushindani mkubwa katika vita ya kuepuka kushuka daraja. Hali hiyo inaweza kuwa hivyo hata bila klabu nyingine kuingizwa ghafla katika mapambano hayo kutokana na sababu kama adhabu za kinidhamu zinazohusiana na masuala ya michezo.