Liverpool yapata mwanya wa kumsajili Barcola
Muktasari:
- Barcola, 23, ni mmoja wa wachezaji wanaowindwa na Liverpool katika dirisha hili la usajili, huku mazungumzo kati ya klabu hizo yakiendelea. Al-Khelaifi amesema hawezi kusema kwa uhakika kama winga huyo ataondoka au la, hali inayofungua zaidi mlango wa uhamisho wake.
LIVERPOOL, ENGLAND: LIVERPOOL imepata matumaini mapya katika harakati zake za kumsajili winga wa Paris Saint-Germain (PSG), Bradley Barcola, baada ya rais wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi, kushindwa kutoa uhakika kwamba mchezaji huyo atasalia Paris msimu huu.
Barcola, 23, ni mmoja wa wachezaji wanaowindwa na Liverpool katika dirisha hili la usajili, huku mazungumzo kati ya klabu hizo yakiendelea. Al-Khelaifi amesema hawezi kusema kwa uhakika kama winga huyo ataondoka au la, hali inayofungua zaidi mlango wa uhamisho wake.
Hali hiyo imeongeza matumaini kwa Liverpool, ambayo inatajwa kuwa tayari imeweka Barcola kwenye orodha yake ya vipaumbele kuelekea msimu mpya.
Zaidi ya hapo, Barcola hakutumika hata dakika moja katika mchezo wa Ngao ya UEFA dhidi ya Aston Villa, ambao PSG ilishinda kwa mabao 2-1 na kutwaa taji hilo kwa mara nyingine. Kutokuwamo kwake uwanjani kumeongeza maswali kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi hicho.
Kwa sasa, bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya Liverpool na PSG, huku tofauti ya thamani ya mchezaji huyo ikiwa ni moja ya vikwazo katika mazungumzo hayo.
Hata hivyo, kauli ya Al-Khelaifi pamoja na Barcola kutotumika dhidi ya Aston Villa vimeongeza dalili kwamba huenda safari yake Paris ikafikia mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa.