Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Liverpool yapanga kuweka mzigo kwa Olise

TETESI Pict

Muktasari:

  • Vigogo hawa wanamwangalia Olide kama mbadala wa Mohamed Salah ambaye huenda akaenda Saudia mwisho wa msimu huu.

LIVERPOOL iko tayari kutumia takribani Pauni 130 milioni kumsajili winga wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, Michael Olise, mwenye umri wa miaka 23, dirisha la majira ya kiangazi mwakani.

Vigogo hawa wanamwangalia Olide kama mbadala wa Mohamed Salah ambaye huenda akaenda Saudia mwisho wa msimu huu.

Olise aliyesajiliwa na Bayern kutoka Crystal Palace kwa Pauni 60 milioni, amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na vigogo hao na msimu huu amecheza mechi 15 za michuano yote, amefunga mabao nane na kutoa asisti nane.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Christoph Freund, amesema anaamini Michael Olise ataendelea kucheza katika klabu hiyo kwa miaka saba na nane ijayo licha ya tetesi zinazosambaa.

Olise ana mkataba wa kuitumikia Bayern hadi mwaka 2029 na klabu hiyo inadaiwa haina mpango wa kumuuza.

Mbali ya uwezo wake wa kufunga Olise amekuwa mmoja wa wachezaji wa Bundesliga wenye asilimia kubwa ya usahihi wa pasi msimu huu, akiwa na asilimia 87.


Rodri

REAL Madrid inapanga kuwasilisha ya takribani Pauni 130 milioni kwenda Manchester City kwa ajili ya kumsajili kiungo wa timu hiyo na Hispania, Rodri, mwenye umri wa miaka 29, dirisha lijalo la majira ya baridi. Rodri amekuwa mhimili wa kiungo wa Man City na kuipa mafanikio makubwa timu hiyo. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Staa huyu alijiunga na Atletico Madrid mwaka 2019 kwa ada ya Pauni 62 milioni.


Harry Maguire

BEKI wa Manchester United, Harry Maguire, 32, anadaiwa huenda akatimkia Saudi Arabia ambako Al-Nassr na Al-Ettifaq zinahitaji huduma yake. Maguire bado ana mwaka mmoja katika mkataba wake na Man United  ina kipengele cha kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa itahitaji kufanya hivyo. Awali Man United ilikuwa tayari kumuuza mwaka jana lakini Maguire mwenyewe alikataa, lakini sasa inadaiwa kuwa tayari.


Ibrahima Konate

LIVERPOOL haipo tayari kumruhusu beki wao wa kimataifa wa Ufaransa, Ibrahima Konate, mwenye umri wa 26, kuondoka Januari licha ya kuhusishwa na Real Madrid. Mkataba wa Konate unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na ikiwa ataendelea kubaki anaweza kuondoka bure lakini Liverpool inaamini atakubali kumsainisha mkataba mpya, hivyo haitaki kumuuza kwa bei rahisi Januari. Madrid wanamwona kama chaguo sahihi la kuwamrithi Antonio Rudiger na David Alaba ambao mikataba yao inakwenda kumalizika.


Etta Eyong

BRENTFORD ipo tayari kulipa Pauni 26 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Villarreal na timu ya taifa ya taifa ya Cameroon, Etta Eyong, mwenye umri wa miaka 21. Eyong amekuwa akifanya vizuri kwenye La Liga msimu huu na hadi sasa amefunga mabao matano katika mechi nane za ligi hiyo. Brentford inaamini staa huyu ataongeza nguvu zaidi katika eneo lao la ushambuliaji.


Nico Schlotterbeck

BARCELONA inataka kuongeza kasi katika juhudi zao za kumsajili beki wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, mwenye umri wa miaka 25, ambaye atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu. Schlotterbeck ni miongoni mwa mabeki bora wa Ujerumani katika miaka ya karibuni na Barca inamwona kama chaguo sahihi lisilo na gharama.



Mike Maignan

BAYERN Munich inataka kuingia katika vita dhidi ya Chelsea ili kuipata saini ya kipa wa AC Milan na timu ya taifa ya Ufaransa, Mike Maignan, mwenye umri wa miaka 30, ili akawe mrithi wa muda mrefu wa Manuel Neuer, mwenye umri wa miaka 39. Maignan, ambaye alijiunga na Milan kutoka Lille mwaka 2021, alikuwa akihitajika na Chelsea tangu dirisha lililopita lakini hakukuwa na mwafaka.


Sergio Reguilon

INTER Miami inayomilikiwa na David Beckham ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kushoto wa zamani wa Tottenham, Sergio Reguilon, mwenye umri wa miaka 28, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na Spurs dirisha lililopita. Reguilon, aliyewahi kuchezea Real Madrid, Sevilla na Manchester United ikiwa atatua Miami ataungana na mastaa wakubwa kama Lionel Messi, Luis Suarez na Jordi Alba.