Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marc Guehi aipa nafasi ya upendeleo Liverpool

TETESI Pict

Muktasari:

  • Kapteni huyu wa Crystal Palace alikuwa karibu kujiunga na Liverpool dirisha lililopita kabla ya dili kufeli dakika za mwisho baada ya kocha wake kuzuia.

BEKI kisiki wa Crystal Palace, Marc Guehi, 25, atakuwa tayari kujiunga na Liverpool ikiwa itawasilisha ofa dirisha lijalo badala ya kusubiria mwisho wa msimu.

Kapteni huyu wa Crystal Palace alikuwa karibu kujiunga na Liverpool dirisha lililopita kabla ya dili kufeli dakika za mwisho baada ya kocha wake kuzuia.

Baada ya dili hilo kufeli ripoti zilieleza Liverpool iliachana na mpango wa kumsajili Januari na badala yake ilihitaji kusubiri hadi mwisho wa msimu. Hata hivyo, hivi karibuni Real Madrid iliibuka na ikatajwa inaweza kuwasilisha ofa ya kumsajili Januari mwakani na ikaripotiwa Guehi mwenyewe amevutiwa zaidi na ofa ya miamba hiyo.

Licha ya tetesi hizo, Geuhi ambaye alishafanya hadi makubaliano binafsi amewapa Liverpool nafasi ya kumpata ikiwa watatuma ofa Januari.

Mkataba wa fundi huyu unamalizika mwisho wa msimu huu na kuna uwezekano Palace ikakubali kumuuza ili asiondoke bure msimu utakapomalizika.


William Saliba

REAL Madrid imeendeleza kumfuatilia beki kisiki wa Arsenal, William Saliba, 24, ili kuipata saini yake dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Madrid inaamini staa huyu atasaidia sana safu yao ya ulinzi na kumekuwa na changamoto ya majeraha ya mara kwa mara kwa wachezaji wao tegemeo. Mkataba wa sasa wa Saliba unamalizika mwaka 2027 na Arsenal imekuwa ikipambana kutaka kumsainisha mkataba mpya lakini hadi sasa hawajafikia mwafaka.


Harry Kane

STRAIKA wa Bayern Munich, Harry Kane, 32, ana kipengele maalum kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuondoka Allianz Arena dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni  56.7  milioni. Hata hivyo, kipengele hicho kitaweza kutumika endapo Kane atatangaza nia ya kuondoka kabla ya dirisha la usajili la msimu Januari kufungwa. Kane, aliyesajiliwa kutoka Tottenham kwa zaidi ya Pauni milioni 100 mwaka 2023, bado ndiye tegemeo kubwa la mabao Bayern lakini kuna tetesi za kurudi England.


Brais Mendez

STRAIKA wa Bayern Munich, Harry Kane, 32, ana kipengele maalum kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuondoka Allianz Arena dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ada ya Pauni  56.7  milioni. Hata hivyo, kipengele hicho kitaweza kutumika endapo Kane atatangaza nia ya kuondoka kabla ya dirisha la usajili la msimu Januari kufungwa. Kane, aliyesajiliwa kutoka Tottenham kwa zaidi ya Pauni milioni 100 mwaka 2023, bado ndiye tegemeo kubwa la mabao Bayern lakini kuna tetesi za kurudi England.


Savinho

TOTTENHAM Hotspur, imepanga kutuma ofa ya kumsajili kwa mkopo winga wa Manchester City, Savinho, 21, kwa mkopo dirisha la Januari mwaka huu. Timu nyingi zilihitaji kumsajili Savinho kwa mkopo dirisha lililopita lakini Man City ilikataa kumuuza ikisisitiza bado ina mipango naye. Hata hivyo, tangu kuanza kwa msimu huu staa huyu amecheza mechi sita za michuano yote, amefunga bao moja na asisti moja.


Nico O’Reilly

CHELSEA imeanza kumfuatilia kwa karibu kiungo wa Manchester City, Nico O’Reilly, 20, ambaye pia anawindwa na Leeds United, Bayer Leverkusen  na Olympique Lyon. Ripoti ya awali iliyowasilishwa na maskauti kwenda benchi la ufundi inadaiwa ilimvutia sana Kocha Enzo Maresca. Mabosi wa Chelsea wapo tayari kutoa zaidi ya Pauni25 milioni kwa ajili ya kumsajili fundi huyu wa kimataifa wa England.


Julian Alvarez

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Julian Alvarez anafikiria kuondoka Hispania dirisha lijalo la majira ya kiangazi na kurejea England na Liverpool inahusishwa kumtaka. Alvarez aliyejiunga na Atletico akitokea Manchester City, anataka kupata changamoto sehemu nyingine. Liverpool inamwona kama chaguo sahihi la kumrithi Mohamed Salah endapo ataondoka.


Marcus Rashford

BARCELONA ipo tayari kutoa Pauni 26 milioni ili kumsainisha mkataba wa moja kwa moja mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford aliyejiunga nao kwa mkopo dirisha lililopita. Mabosi wa Barca wanataka kutoa kiasi hicho ambacho ni pungufu ya kile kilichopo katika mkataba wa Rashford ambao unaeleza ikiwa wanahitaji huduma yake watatakiwa kutoa Pauni 35 milioni.