Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi wa Real Madrid wapanga hili kwa Konate

TETESI Pict

Muktasari:

  • Vigogo hao wanaona itakuwa wamechelewa sana endapo watasubiri hadi mwisho wa msimu kwa sababu wana uhitaji wa kuboresha eneo lao la ulinzi haraka iwezekanavyo.

MABOSI  wa juu wa Real Madrid wanafikiria kuachana na mpango wa kuendelea na mazungumzo ya kumsajili beki wa  Liverpool na timu ya taifa ya Ufaransa, Ibrahima Konate, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na badala yake wanafikiria kusajili beki mwingine katika dirisha lijalo la Januari.

Vigogo hao wanaona itakuwa wamechelewa sana endapo watasubiri hadi mwisho wa msimu kwa sababu wana uhitaji wa kuboresha eneo lao la ulinzi haraka iwezekanavyo.

Awali, ilielezwa kuwa Madrid inataka kumsajili Konate pale mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwisho wa msimu huu na mchezaji mwenyewe ameshakubali kujiunga nao.

Madrid imekuwa ikipitia changamoto kubwa katika eneo la ulinzi ambalo mastaa wengi wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Liverpool imekuwa ikijaribu kufanya mazungumzo ya kumpa mkataba mpya Konate lakini hayuo tayari kubakia.

Konata amecheza zaidi ya mechi 95 akiwa na Liverpool na kushinda FA Cup 2022 , Carabao Cup 2022 & 2024 na Ligi Kuu England msimu uliopita.


Maxence Lacroix

LIVERPOOL inafikiria kumsajili beki wa Crystal Palace, Maxence Lacroix baada ya kuona uwezekano wa kumpata beki mwingine wa timu hiyo, Marc Guehi unaonekana kuwa mgumu siku hadi siku.

Lacroix ambaye alitua Palace mwaka jana akitokea Wolfsburg amekuwa sehemu muhimu ya safu ya ulinzi ya Palace akishirikiana na Guehi.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na Palace inaripotiwa kuwa tayari kumuuza lakini kwa zaidi ya Euro 40 milioni.


Yehor Yarmolyuk

MANCHESTER United imeongeza jina la kiungo wa Brentford na timu ya taifa ya Ukraine, Yehor Yarmolyuk, mwenye umri wa miaka 21, katika orodha ya wachezaji inaotaka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Yarmolyuk alijiunga na Brentford mwaka 2022 kutoka Dnipro-1 ya Ukraine na msimu uliopita alicheza mechi 34 za michuano yote.

Staa huyu anaonekana kama mbadala wa muda mrefu wa Casemiro anayeweza kuondoka.


Joshua Zirkzee

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, ambaye hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha mashetani wekundu anawindwa na Juventus na AC Milan zinazotaka kumsajili jumla wakati Como nayo ikimtaka lakini kwa mkopo wa nusu msimu.

Zirkzee ambaye pia ana uraia wa Nigeria, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi nne tu ambazo zote aliingia akitokea benchini.


Hayden Hackney

TOTTENHAM Hotspur na Manchester United zipo mbele ya Fulham katika mbio za kumsajili kiungo wa Middlesbrough, Hayden Hackney, mwenye miaka 23.

Hackney aling’ara sana msimu uliopita katika Ligi Daraja la Kwanza nchini England akicheza mechi 40 na kutoa asisti 10. Mabosi wa Middlesbrough wanahitaji takribani Pauni 35 milioni ili kumuuza staa huyu katika dirisha lijalo.


Oihan Sancet

WAWAKILISHI wa Newcastle United wanatarajiwa kutua Hispania ndani ya wiki kadhaa zijazo kwa ajili ya kumtazama kiungo wa Athletic Bilbao, Oihan Sancet, 25, kabla ya kuanza rasmi mazungumzo ya kuipata saini yake katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Staa huyu alikuwa mmoja kati ya wachezaji waliowezesha Bilbao kushinda taji la Copa del Rey mwaka 2024.


Warren Zaire-Emery

REAL Madrid inataka kuhamia kwa kiungo chipukizi wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Warren Zaire-Emery, mwenye umri wa miaka 19, baada ya kuona uwezekano wa kumpata Rodri kutoka Manchester City ni mgumu na sasa na hata ikiamua kuweka pesa haitaweza kumtumia kwani anasumbuliwa na majeraha kwa sasa.

Warren tayari amecheza timu ya taifa ya wakubwa ya Ufaransa, akifanikiwa kufunga bao kwenye mechi yake ya kwanza.


Erling Haaland

STRAIKA wa Manchester City, Erling Haaland anadaiwa kushindwa kuvumilia juu ya kile kinachoendelea katika timu yake na anafikiria kuondoka ifikapo mwisho wa msimu huu.

Haaland ambaye ana mkataba hadi mwaka 2034, huenda akakubali ofa ya kujiunga na Barcelona au Real Madrid ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaj huduma yake kwa muda mrefu.

Hata hivyo, changamoto kubwa inaweza kuwa ada yake ya uhamisho inayodaiwa kufikia Euro 100 milioni.