Liverpool kukipiga Tottenham Carabao Cup
Muktasari:
- Katika michezo mingine, Manchester United itamenyana na Brighton & Hove Albion, wakati mabingwa watetezi Manchester City watakuwa wenyeji wa Norwich City.
LONDON, ENGLAND: LIVERPOOL imepangwa kukutana na Tottenham Hotspur katika raundi ya tatu ya Carabao Cup, huku timu tisa za Ligi Kuu England zinazoshiriki michuano ya Ulaya zikianza kampeni zao katika hatua hiyo.
Katika michezo mingine, Manchester United itamenyana na Brighton & Hove Albion, wakati mabingwa watetezi Manchester City watakuwa wenyeji wa Norwich City.
Arsenal itasafiri kucheza na Ipswich Town, huku Aston Villa ikikabiliana na Coventry City.
Timu nyingine zitakazokutana ni Crystal Palace dhidi ya Middlesbrough, Sunderland dhidi ya Hull City na Bournemouth dhidi ya Lincoln City.
Timu zote tisa za Ligi Kuu zinazoshiriki mashindano ya Ulaya msimu huu Arsenal, Aston Villa, Bournemouth, Brighton, Crystal Palace, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Sunderland zimeanza Carabao Cup moja kwa moja kutoka raundi ya tatu.
Ili kuepusha mgongano wa ratiba na hatua za mwanzo za Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League, michezo hiyo itachezwa katika wiki zinazoanza Jumatatu, Septemba 7 na Jumatatu, Septemba 14.
Mechi mbili za mwisho za raundi hiyo zitaamuliwa Alhamisi, Chelsea itakapomenyana na Luton saa 1:30 usiku, huku Fulham ikicheza na AFC Wimbledon saa 2:00 usiku.
Droo kamili ya raundi ya tatu
Crystal Palace vs Middlesbrough
Manchester United vs Brighton
Manchester City vs Norwich
Sunderland vs Hull City
Ipswich Town vs Arsenal
Coventry City vs Aston Villa
Bournemouth vs Lincoln City
Liverpool vs Tottenham
Chelsea au Luton vs Leeds United
Millwall vs Newcastle United
Fleetwood Town vs Sheffield United
Everton vs Wolverhampton Wanderers
Leyton Orient vs Bradford City
Reading vs Brentford
Peterborough United vs Barnsley
West Ham United vs Fulham au AFC Wimbledon