Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Leipzig yaipa Arsenal bei kwa Sesko

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa michezo wa Leipzig, Marcel Schafer, na Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, wanaripotiwa kukutana na kujadili kuhusu za ada ya uhamisho  ambapo Leipzig inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 75 milioni kwa ajili ya staa huyo mwenye umri wa miaka 21.

LONDON,ENGLAND: ARSENAL na Red Bull Leipzig wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mshambuliaji wa timu hiyo, Benjamin Sesko.

Mkurugenzi wa michezo wa Leipzig, Marcel Schafer, na Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal, Andrea Berta, wanaripotiwa kukutana na kujadili kuhusu za ada ya uhamisho  ambapo Leipzig inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 75 milioni kwa ajili ya staa huyo mwenye umri wa miaka 21.

Arsenal wanahitaji kuboresha kikosi chao kuelekea dirisha lijalo na moja kati ya maeneo ambayo imeyapa kipaumbele ni  kupata mshambuliaji mpya.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, hivi karibuni alikiri kuwa timu hiyo huenda ikavunja rekodi yao ya usajili ili kuimarisha safu ya ushambuliaji.

"Bajeti ni kama unapopanga harusi, unapanga harusi na mke wako, unampa bajeti lakini haitoshi kamwe, huwa inaongezeka. Unapojenga nyumba, bajeti huwa inaongezeka. Kwa kawaida mambo hayo hutokea.

Kuna vitu vingi vinavyoweza kutokea, lakini huwa tunapanga bajeti na tunajua kile ambacho tunaweza kufanya."

Arsenal pia wamezungumza na Sporting Lisbon kwa ajili ya  mshambuliaji Viktor Gyokeres ambaye pia inahitaji huduma yake.

Kwa upande wa wachezaji wanaoondoka, winga wa Arsenal, Marquinhos, amejiunga na Cruzeiro.

Mchezaji huyo wa Kibrazili alijiunga na Arsenal mwaka 2022 lakini alicheza mechi moja pekee kabla ya kutolewa kwa mkopo mara kadhaa.