Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda ajipa matumaini Simba

Muktasari:

  • Mgunda alisajiliwa na Simba dakika za mwisho kabisa za dirisha la usajili lilipita na hadi sasa bado hajapata nafasi ya kuonyesha makali yake kwenye kikosi hicho cha Msimbazi.

INGAWA mshambuliaji wa Simba, Ismail Mgunda bado hajaanza kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, amesema wachezaji wanaocheza nafasi yake wapo vizuri na wanampa chachu nzuri ya kuendelea kujituma kwa bidii, akiamini bado zimesalia mechi nyingi atacheza muda ukifika.

Mgunda alisajiliwa na Simba dakika za mwisho kabisa za dirisha la usajili lilipita na hadi sasa bado hajapata nafasi ya kuonyesha makali yake kwenye kikosi hicho cha Msimbazi.

Kati ya wachezaji aliowataja Mgunda ni Elie Mpanzu ambaye kwa sasa Ligi Kuu anamiliki mabao matano, asisti tatu na michuano ya CAF alifunga mabao mawili dhidi ya 15 de Agosto.

“Simba ina wachezaji washindani wa namba kila nafasi, nimejiunga nimewakuta kina Mpanzu, wanaonyesha kiwango cha juu hiyo ni chalenji kwangu, kuendelea kujituma na kupambana kwa bidii kuhakikisha napata nafasi ya kucheza, bado zipo mechi nyingi msimu haujaisha,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Mpanzu ni mtu ninayezungumza naye sana, kuna wakati tunawekeana chalenji ya kufunga mabao katika mazoezi, siyo huyo tu na watu wengine, lakini mwisho wa siku mechi hamuwezi kuanza wote, kocha anayemuona yupo vizuri anakuwa anamwanzisha ili kusaidia timu.”

Tangu ajiunge Simba, amecheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) dhidi ya Mighty Wanderers, timu hiyo ilishinda kwa mabao 6-1, iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Septemba 13, 2026.

Mgunda aliingia dakika ya 79 akichukua nafasi ya Mpanzu na dakika ya 88 alitoa pasi ya bao lililofungwa na Keletso Makgalwa, lakini kwa mechi za Ligi Kuu aliingia kipindi cha pili dhidi ya Mashujaa FC, Wanamsimbazi wakishinda kwa mabao 6-1.

Takwimu zake: msimu wa 2023/24 katika Ligi Kuu akiwa Singida BS alimaliza na mabao sita, wakati alipokuwa Mashujaa 2024/25 alimaliza na mabao mawili na 2025/26 mabao mawili, msimu huu unaoendelea wa 2026/27 bado hajafungua akaunti ya mabao Ligi Kuu.

Pamoja na kutoanza kufunga lakini amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa wachezaji wa zamani ambao, Steven Mapunda alisema mshambuliaji huyo ana faida kubwa kama Simba watamvumilia.

Mgunda ana faida kubwa,  ana uwezo wa kukaa na mpira mguuni pia kuutafuta pindi unapokuwa kwa wapinzani, inaweza ikawa ngumu kuona moja kwa moja anafunga mabao mengi, lakini ana faida nyingine zaidi, kama ilivyokuwa kwa Kibu Denis hakuwa anafunga mabao mengi ila alikuwa na faida zingine zaidi kama mikimbio yake iliyokuwa inawapa presha wapinzani, nguvu na wakati mwingine kukaba.”