Kombe la Dunia la Klabu moto wazidi kuwashwa

Muktasari:
- Timu kubwa kutoka mabara tofauti kama Fluminense, Borussia Dortmund, Al Ahly na Urawa Red Diamonds zitashuka dimbani kuwania pointi muhimu.
FLORIDA, MAREKANI: USIKU wa leo, kuanzia saa sita wakati siku inabadilika na kuwa Juni 17, Kombe la Dunia la Klabu litaendelea kwa michezo minne ya hatua ya makundi.
Timu kubwa kutoka mabara tofauti kama Fluminense, Borussia Dortmund, Al Ahly na Urawa Red Diamonds zitashuka dimbani kuwania pointi muhimu.
Hapa tumekushushia uchambuzi na rekodi juu ya timu zote zitakazoshuka dimbani kuvaana katika michuano hii inayoshirikisha jumla ya timu 32.

FLUMINENSE vs BORUSSIA DORTMUND
Muda: Leo Saa 1:00 usiku
Uwanja: MetLife Stadium, East Rutherford, Marekani
Fluminense ya Brazil inashiriki michuano hii kwa mara ya pili, baada ya kwa mara ya kwanza mwaka 2023 na ilifika hatua ya fainali na ikapoteza mbele ya Manchester City ya England.
Kwa upande wa Borussia Dortmund ya Ujerumani hii ni mara yao ya kwanza kushirki michuano hii ingawa ina uzoefu mkubwa wa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mara ya mwisho kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa mwaka 1997 na michuano ilianzishwa mwaka 2000.

ULSAN HYUNDAI vs MAMELODI SUNDOWNS
Muda:Leo Saa 7:00 usiku.
Uwanja: Inter&Co Stadium, Orlando, Marekani
Ulsan Hyundai ya Korea Kusini ni mabingwa mara mbili wa Ligi ya Mabingwa Asia. Inashiriki michiano hii kwa mara ya tatu. Mara ya mwisho ni mwaka 2020 na kumaliza nafasi ya sita. Ina historia ya ushindani wa hali ya juu katika Bara la Asia, lakini hawajawahi kufika mbali katika michuano hii.
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini inashiriki kwa mara ya pili baada ya mwaka 2016 na kumaliza nafasi ya sita pia. Wawakilishi hawa wa Afrika wameimarika sana katika miaka ya hivi karibuni na msimu uliopita walipoteza fainali ya Ligi ya Mabingwa mbele ya Pyramid FC.

RIVER PLATE vs URAWA RED DIAMONDS
Muda: Leo Saa 4:00 usiku
Uwanja: Lumen Field, Seattle, Marekani
River Plate ya Argentina inarejea kwenye Club World Cup ikiwa na kumbukumbu ya kushiriki mwaka 2015 na ilifika fainali na ilifungwa na Barcelona. Hii ni mara yao ya pili kushiriki na inakuja ikiwa na kikosi chenye uzoefu mkubwa wa kimataifa.
Urawa Red Diamonds ya Japan hii ni michuano yao ya nne kushiriki na hapo awali ilipata mafanikio ikiwemo kumaliza nafasi ya tatu mwaka 2007 na kuishia fainali mwaka 2023.

MONTERREY vs INTER MILAN
Muda: Kesho saa 10:00 alfajiri
Uwanja: Rose Bowl, Pasadena, Marekani
Monterrey ya Mexico, hii ni mara yao ya sita tangu ilipoanza kushiriki mwaka 2011. Ilifanya vizuri mwaka 2019 na 2021 ilipomaliza nafasi ya tatu. Ina uzoefu mkubwa na inajua presha ya michuano hii.
Inter Milan ya Italia zinashiriki kwa mara ya pili katika historia yao. Mara ya kwanza ilishiriki mwaka 2010 na ikachukua taji. Inarudi ikiwa na kikosi kipya chini ya kocha mpya Cristian Chivu ambaye amechukua mikoba ya Simone Inzaghi aliyetimkia Al-Hilal.

BENFICA vs BOCA JUNIORS
Muda: Leo Saa 7:00 usiku
Uwanja: Estádio Metropolitano (Virtual/Friendly Match Venue)
Hii ni mara ya kwanza kwa Benfica kushiriki mashindano haya lakini itakumbana na Boca ambayo ina uzoefu wa kutosha kwani imewahi kushiriki mara tatu.
Katika mara tatu ilizoshiriki Boca imefika fainali zote, ikishinda mara moja dhidi ya Real Madrid mwaka 2000.
Ikafungwa fainali na Bayern mwaka 2001 pia ikapoteza fainali nyingine dhidi ya AC Milan mwaka 2007.

FLAMENGO vs SPERANCE DE TUNIS
Muda: Leo Saa 10:00 Alfajiri
Uwanja: Lincoln Financial Field, Philadelphia
Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Flamengo kushiriki michuano hii na mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2019 na ilimaliza nafasi ya tatu, baada ya kuichapa Al Ahly mabao 4‑2 kwenye michuano iliyofanyika huko Morocco.
Mara yao yapili kushiriki ilikuwa mwaka 2022 na ikaishia hatua ya nusu fainali.
Esperance de Tunis yenyewe inashiriki kwa mara yao ya nne baada ya kuonekana mwaka 2011, 2018 na 2019.
Licha ya kushiriki mara zote hizo, haijawahi kupenya hata nusu fainali.