Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha: Mbeumo anajipa presha mwenyewe

MBEUMO Pict

Muktasari:

  • Mbeumo, aliyebadili uraia wa kimichezo baada ya kuichezea Ufaransa katika ngazi za vijana, amebeba matumaini ya Cameroon katika AFCON iliyoingia hatua ya 16 Bora huku wakisaka taji lao la kwanza la Afrika tangu mwaka 2017.

CASABLANCA, MOROCCO: KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, David Pagou amesema mshambuliaji Bryan Mbeumo anapenda kucheza kwa uhuru, lakini kwa sasa anajiwekea presha kubwa sana katika harakati za kufanya vizuri kwenye michuano ya  Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea huko Morocco.

Mbeumo, aliyebadili uraia wa kimichezo baada ya kuichezea Ufaransa katika ngazi za vijana, amebeba matumaini ya Cameroon katika AFCON iliyoingia hatua ya 16 Bora huku wakisaka taji lao la kwanza la Afrika tangu mwaka 2017.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anayeichezea Manchester United alitoa pasi ya bao kwa mabingwa hao mara tano wa Afrika katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Gabon katika mechi ya kwanza, na alikuwa hajafunga bao katika michuano hiyo ya 35 kabla ya mechi ya usiku wa jana dhidi ya Msumbiji.

“Anajiwekea presha kubwa sana, lakini naamini ataweza kuidhibiti. Ni mchezaji mkubwa, mchezaji bora, hata kwa taifa hili. Anaipenda timu hii na anataka kujitoa kwa kiwango cha juu zaidi,” amesema Pagou alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mechi ya usiku wa jana kukamilisha hatua ya makundi.

“Leo tena, katika mazungumzo yetu mafupi naye, bado ana kiu ya kuwapo, kuchukua jukumu, na kufanya mambo makubwa.”

Mbeumo amecheza mechi 29 za kimataifa na kufunga mabao saba.

“Bryan ni mchezaji anayependa uhuru wa kucheza; ana sifa hizo. Hivyo hatutamnyima uhuru huo wala kumzuia kujieleza uwanjani kwa mtindo anaoupenda,” amesema Pagou.

“Ndiyo maana tunamruhusu kucheza maeneo mbalimbali ya uwanja. Ni kweli kwamba amekuwa na changamoto kidogo katika kuonyesha kiwango chake bora.”

Cameroon walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Ivory Coast katika mechi ya pili ya Kundi F na jana Jumatano ilitarajiwa kukutana na Msumbiji, huku zote zikiwa zimeshafuzu 16 Bora pamoja na Ivory Coast iliyokuwa ikicheza na Gabon.