Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amad Diallo amewasha moto Ivory Coast

AMAD Pict

Muktasari:

  • Mbeumo aliasisti kwenye mechi ya kwanza ya Cameroon katika hatua ya makundi, wakati Amad alifunga bao pekee kuipa ushindi Ivory Coast kwenye mechi yao ya kwanza pia katika mashindano hayo ya Afcon 2025.

RABAT, MOROCCO: MASTAA wawili wa Manchester United, Amad Diallo na Bryan Mbeumo wamekumbana uwanjani jino kwa jino kwenye mashindano ya Afcon 2025 huko Morocco.

Mbeumo aliasisti kwenye mechi ya kwanza ya Cameroon katika hatua ya makundi, wakati Amad alifunga bao pekee kuipa ushindi Ivory Coast kwenye mechi yao ya kwanza pia katika mashindano hayo ya Afcon 2025.

Amad ametua kwenye michuano hiyo kwa kishinda, ambapo amefunga mabao mawili katika mechi mbili alizocheza.

Winga huyo, Amad alipokea mpira akiwa pembeni wakati Ivory Coast inafanya shambulizi la kushtukiza dhidi ya Cameroon.

Aliwatambuka mabeki kadhaa wa Simba Wasioshindika kabla ya kupiga shuti maridadi kabisa kwa mguu wa kushoto, mpira ukitinga kwenye kona kabisa ya goli, akiitanguliza Tembo kwa bao 1-0.

AMA 01

Amad aliendelea kuwa tishio kwa Cameroon, akipiga mashuti matano golini, huku mawili yakizuiwa na mabeki. Staa huyo alikuwa kwenye kiwango bora kabisa, akipiga pasi nne matata kabisa za kuleta mabao, huku akitengeneza nafasi moja kubwa ya mashambulizi. Katika mechi hiyo, alipiga krosi nne, huku mambo mengine mengi yakiwa bora kabisa kwa upande wake.

Kwenye ishu ya kusaidia kukaba, Amad alishinda bato mbili za kunyang'anya mipira, huku pia alikuwa na asilimia 100 ya mafanikio ya kunasa mipira kwenye miguu ya wapinzani katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Simba Wasioshindika.

Amad na chama lake la Ivory Coast litacheza mechi yao ya mwisho kwenye hatua ya makundi dhidi ya Gabon, Desemba 31.

Amad katika pasi 22 alizopiga, 21 zilikuwa sahihi, huku pasi 13 kati ya 14 alizopiga kwenye nusu ya goli la wapinzani zilikuwa sahihi na aligusa mpira mara 41.

Kuhusu Mbeumo, hakuwa na vitu vitamu tofauti mchezaji mwenzake, lakini alikuwa muhimu kwa upande wa Cameroon.

AMA 02

Alipiga mashuti matatu golini, moja likizuiwa na mabeki wa Ivory Coast.

Alifanya jaribio la kupiga chenga na kufanikiwa, huku akipiga krosi moja na muda mwingi aliifanya ngome ya mabeki wa Ivory Coast kuwa kwenye shaka kubwa.

Alisaidia pia kwenye ulinzi, ambapo alishinda vita tatu za kugombea mpira, huku akinyang'anya mipira mara mbili kutoka kwenye eneo la mabeki.

Cameroon itacheza mechi yake ya mwisho ya makundi dhidi ya Msumbiji katika Mkesha wa Mwaka Mpya.

Amad alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo, lakini wakati anakwenda kupokea tuzo, alivaa jezi ya Mbeumo akiwa na maana kwamba mchezaji mwenzake huyo wa Old Trafford, naye aliyestahili tuzo hiyo kwa kile alichofanya uwanjani.