Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kimeumana… Ligi Kuu England moto unawaka

EPL Pict

Muktasari:

  • Timu hizo ziliibuka na ushindi wa mabao 2-1, Arsenal ikifanya hivyo dhidi ya Brighton, Manchester City ikaichapa Nottingham Forest, na Aston Villa ikaipiga Chelsea.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya timu zote tatu zinazoshika nafasi za juu katika Ligi Kuu England kushinda mechi zao Jumamosi, vita ya kuliwania taji la ligi hiyo msimu huu imeendelea kupamba moto.

Timu hizo ziliibuka na ushindi wa mabao 2-1, Arsenal ikifanya hivyo dhidi ya Brighton, Manchester City ikaichapa Nottingham Forest, na Aston Villa ikaipiga Chelsea.

Baada ya mechi 18, ambazo kila timu imecheza hadi sasa, Mikel Arteta na vijana wake bado wameendelea kukaa kileleni wakiwa na pointi 42, pointi mbili mbele ya Man City na tatu mbele ya Villa.

Msimu bado ni mrefu na kuna mambo kadhaa yanaonekana kuwa huenda yakaamua timu ipi itakayokuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuchukua ubingwa  msimu huu.

Moja kati ya maeneo ambayo yanaonekana kuwa yataamua ubingwa ni mechi kati ya Arsenal na Villa inayotarajiwa kupigwa kesho.

Arsenal ilitoa sare katika mechi ya mzunguko wa kwanza msimu huu dhidi ya Villa na hiyo ilichangia sana kupunguza utofauti wa alama kati yao na Man City.

Vijana hawa wa Arteta wamekuwa wakipambana na kukaribia kuchukua ubingwa kwa misimu mitatu sasa, lakini mara kadhaa mechi dhidi ya Villa huwa inawarudisha sana nyuma na muda mwingine kuwapandisha.

Ushindi wao wa mabao 4-2 mwaka 2023 ulibadilisha kila kitu na kuwafanya kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda taji kabla ya mambo kuharibika mwishoni.

EP 01

Vilevile, kipigo kutoka wa Villa mwaka 2024 wakati ikielekea ukingoni kilichangia sana wao kushindwa kupata taji la ligi msimu huo.

Eneo la pili ni usajili wa dirisha la Januari linalokaribia kufunguliwa. Timu hizi tatu zimefaidika na usajili wa Januari katika misimu iliyopita. Wachezaji kama Leandro Trossard, Jorginho na Jakub Kiwior walisaidia kuboresha kikosi cha Arsenal mwaka 2023, pia Man City ilifaidika na mastaa kama Omar Marmoush na Nico Gonzalez.

Villa pia ilifaidika sana na usajili wake wa dirisha la Januari mwaka huu ambapo iliwachukua kwa mkopo Marco Asensio na Marcus Rashford na baada ya hapo ikafanikiwa kuvuna pointi 29 katika mechi 14, hali iliyowafanya kufuzu michuano ya kimataifa.

Katika dirisha hili Man City inaonekana kutaka kumsajili Antoine Semenyo, ambaye usajili wake unaweza kugharimu Pauni 65 milioni.

Hadi sasa Villa haijajulikana ni wachezaji gani haswa inawapa kipaumbele zaidi ingawa kuna majina ya wachezaji wengi wanaohusishwa kuwa wanaweza kuwasajili.

Eneo la majeruhi pia linaweza kuamua mbio hizi. Arsenal haikuwa na Jurrien Timber na Riccardo Calafiori katika mechi yao dhidi ya Brighton, huku Ben White na Cristhian Mosquera pia wakikosekana.

Hata hivyo, Kai Havertz yupo karibu na kurejea na beki Gabriel Magalhaes amepona.

Man City inamkosa staa wake Omar Marmoush na Rayan Ait-Nouri ambao  wanazitumikia timu zao katika michuano ya AFCON, lakini John Stones na Jeremy Doku wanaweza kurudi mapema baada ya kuanza mazoezi mepesi.

Villa pia inawakosa baadhi ya wachezaji, ikiwamo Evann Guessand, aliyeitwa kwenye AFCON kuitumikia Ivory Coast.


MECHI ZIJAZO

ARSENAL

Villa

Bournemouth (a),

 Liverpool (h),

 Nottingham Forest (a)

Manchester United (h)

MAN CITY

Sunderland

 Chelsea (h)

 Brighton (h)

 Man Utd (a)

 Wolves (h)


ASTON VILLA

Arsenal

 Nottingham Forest (h),

 Crystal Palace (a),

 Everton (h)

Newcastle (a)