Kaamua! Ilikuwa Shoo ya Moreira Derby della Madonnina
Muktasari:
- Katika mechi ambayo nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyezaliwa Agosti 6, 2004 alikuwa akihaha kila kona ya uwanja, alifunga bao la kuvutia kwa mpira wa adhabu na kutoa pasi mbili za mabao, huku Milan ikimaliza mwanzo mzuri wa Inter katika msimu wa Serie A kwa ushindi ambao awali haukutarajiwa.
MILAN, ITALIA: DIEGO Moreira alitoa asisti mbili na kufunga bao moja, akiiongoza AC Milan kuibuka na ushindi katika mchezo wa Dabi ya Milan maarufu Derby della Madonnina dhidi ya Inter Milan kwenye Ligi Kuu Italia (Serie A), mechi iliyomalizika jina lake likiimbwa hadi mitaani na mashabiki wa timu yake. Milan iliichapa Inter kwa mabao 3-1.
Katika mechi ambayo nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji aliyezaliwa Agosti 6, 2004 alikuwa akihaha kila kona ya uwanja, alifunga bao la kuvutia kwa mpira wa adhabu na kutoa pasi mbili za mabao, huku Milan ikimaliza mwanzo mzuri wa Inter katika msimu wa Serie A kwa ushindi ambao awali haukutarajiwa.
Mchezaji huyo alihitaji dakika 10 pekee kuandaa mabao ya Christian Pulisic na Adrien Rabiot, huku kikosi hicho cha kocha wa zamani wa Manchester United, Ruben Amorim kikianza kwa kasi kubwa katika Uwanja wa San Siro. Ingawa bao la kwanza la Alessandro Bastoni katika mechi 20 za dabi liliirudisha Inter mchezoni katikati ya kipindi cha kwanza, Moreira aliifanya Milan kuondoka mbali.
Bao la kuvutia la Moreira kwa mpira wa adhabu dakika ya 43 liliirejeshea Milan uongozi wa mabao mawili, ambao hawakuupoteza hadi mwisho, huku Inter ikishindwa kupata nafasi ya kurudi mchezoni katika kipindi cha pili.
Moreira, aliyerejea kwenye kikosi baada ya kukosa mechi ya dhidi ya Bologna iliyomalizika kwa kipigo cha 4-2 kutokana na majeraha, alihitaji dakika nne tu kuonyesha uwezo.
Baada ya kufika karibu na mstari wa mwisho upande wa kulia, alirudisha mpira nyuma na kupiga krosi ya mguu wa kushoto iliyomfikia Pulisic, ambaye aliupiga kwa kichwa na kuuweka kwenye kona ya chini kushoto ya lango.
Rossoneri hawakusubiri muda mrefu kupata bao la pili, ambalo lilitokana moja kwa moja na mazoezi ya timu. Moreira alipiga kona ya chini iliyomfikia Rabiot, ambaye alipiga mpira kwa ustadi juu ya kipa na kugonga nguzo ya mbali kabla ya kuingia wavuni.
Inter ilipunguza pengo kwa bao la mpira wa adhabu dakika ya 22. Bastoni alifunga kwa kichwa baada ya mpira wa kona wa Hakan Calhanoglu kuguswa na Manuel Akanji, na ni kuokoa kwa kiwango cha juu kwa Mike Maignan pekee kulikomzuia Djed Spence kusawazisha muda mfupi baadaye.
Hata hivyo, Moreira alihakikisha Rossoneri inaingia mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao mawili, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kupiga mpira wa adhabu kwa mguu wa kushoto uliopinda kwa ustadi na kumpita Josep Martínez kutoka umbali wa mita 20.
Baada ya Moreira kumtesa Carlos Augusto katika kipindi cha kwanza, ilikuwa jambo la kushangaza kumuona mchezaji huyo akianza kipindi cha pili, lakini alishindwa kutumia vizuri nafasi ya mpira wa kichwa dakika ya 56.
Inter ilipata matumaini ya kupunguza pengo hadi bao moja baada ya mwamuzi Marco Guida kuonyesha alama ya penalti kutokana na madai ya mpira kumgonga mkono Mario Gila.
Hata hivyo, mapitio ya VAR yalimwondolea lawama Mhispania huyo haraka, baada ya marudio kuonyesha kuwa krosi ya Henrikh Mkhitaryan iligonga kifua chake. Kuanzia hapo, Inter ilishindwa kuonyesha uwezo wa kutosha katika mashambulizi, huku mpira wa Ange-Yoan Bonny uliozuiwa ukiwa ndiyo mchango wao mkubwa zaidi.
MWAMBA MOREIRA
Dabi chache duniani zimewashirikisha wachezaji wengi wenye historia kubwa katika soka kama hii, na katika mechi kubwa zaidi, Moreira alilitangaza jina lake kwa kiwango cha kukumbukwa.
Baada ya kuandaa mabao mawili ya haraka yaliyoipa Milan msingi wa ushindi, winga huyo alichukua mpira kutoka kwa Pulisic na Luka Modric kwa kujiamini na kufunga la tatu moja kwa moja kwa mpira wa adhabu lililofungwa na mchezaji wa Rossoneri katika Derby della Madonnina tangu 2004-05.
Andrea Pirlo aliwahi kufunga bao la mpira wa adhabu dhidi ya Inter katika mechi ya Serie A Desemba 2007, huku Theo Hernandez akifanya hivyo katika Supercoppa Italiana Januari 2025.
Kiwango cha Moreira kiliifanya San Siro kung’ara, katika uwanja maarufu ambao muda wake wa kutumika unaelekea ukingoni, baada ya Milan na Inter kutangaza mipango ya kujenga uwanja mpya wa pamoja, Generali Stadium, wiki iliyopita.
Hata hivyo, Moreira hakuwa mchezaji pekee wa Milan aliyechangia kwa kiwango kikubwa. Rabiot sasa amefunga au kutoa pasi ya bao katika kila moja ya mechi zake tano za mwisho za Serie A (mabao manne na asisti mbili), na kuwa kiungo wa tatu kufikia kiwango hicho kwa Milan tangu mwanzo wa msimu wa 2004-05, baada ya Kaka na Calhanoglu.
AC Milan sasa imeshinda mechi tatu mfululizo za Serie A dhidi ya wapinzani wao kwa mara ya kwanza tangu Carlo Ancelotti alipoiongoza timu hiyo kupata ushindi mara nne mfululizo kati ya 2002 na 2004. Katika mashindano yote, Milan haijafungwa katika mechi nane dhidi ya Inter (imeshinda sita na sare mbili).