Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jay-Z, Roc Nation wajitosa sakata la mtoto Nevada

JAY Z Pict

Muktasari:

  • Tukio hilo limezua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wakihusisha kilichotokea na ubaguzi wa rangi kwa kuwa Nevada ni mtoto mweusi.

KAMPUNI ya usimamizi wa vipaji vya michezo, Roc Nation Sports, inayomilikiwa na msanii Jay-Z, imetangaza kumuunga mkono Nevada Pierre, mtoto wa miaka mitatu ambaye kipaji chake cha soka kimevuta hisia za watu wengi duniani kupitia mitandao ya kijamii.

Hatua hiyo imekuja baada ya picha na video za Nevada zikionyesha uwezo wake wa kucheza soka kusambaa kwa kasi mtandaoni na kuwavutia mashabiki. Roc Nation Sports imempongeza mtoto huyo, ikimtaja kuwa ni “nyota inayong’aa” na kuahidi kumuunga mkono katika safari ya kukuza kipaji chake.

Umaarufu wa Nevada uliongezeka zaidi baada ya tukio lililozua mjadala kuhusu namna alivyotendewa wakati wa mchezo wa watoto uliofanyika Oktoba 24, 2026, katika mji wa Winter Park, Florida, Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa, mtoto huyo aliondolewa uwanjani kwa amri ya polisi baada ya wazazi wa baadhi ya watoto aliokuwa akicheza nao kulalamika kuhusu namna alivyotawala mchezo na kufunga mabao mengi dhidi ya timu pinzani.

Tukio hilo limezua hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wakihusisha kilichotokea na ubaguzi wa rangi kwa kuwa Nevada ni mtoto mweusi.

Uamuzi wa Roc Nation Sports kujitokeza kumuunga mkono Nevada umeongeza matumaini kwa mashabiki wanaotaka kuona kipaji chake kikikuzwa. Msaada huo unaweza kuwa hatua muhimu kwa mtoto huyo na familia yake, huku safari yake ya soka ikiwa bado changa kutokana na umri wake mdogo.