Tukio la Nevada laishtua dunia
Muktasari:
- Tukio hilo lilitokea Oktoba 24, 2026, katika mji wa Winter Park, Jimbo la Florida, Marekani.
Tukio la mtoto wa miaka mitatu (Nevada Pierre) kuondolewa uwanjani na polisi kwa kuwapiga chenga na kuwanyanyasa wenzake kisoka, limeibua hisia kali duniani huku likihusishwa na suala la ubaguzi wa rangi.
Mtoto huyo alilazimika kuondolewa uwanjani kwa amri ya polisi baada ya wazazi wa watoto waliokuwa wakicheza naye kuchukizwa na kitendo chake cha kumiliki mpira kila wakati na kuifunga timu pinzani mabao mengi.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 24, 2026, katika mji wa Winter Park, Jimbo la Florida, Marekani.
Hali hiyo imewagusa watu wengi duniani kote, huku mashabiki mtandaoni wakihusisha tukio hilo na ubaguzi kutokana na mtoto huyo kuwa mweusi.
Baada ya sakata hilo, kampeni kubwa ya kuchangisha fedha ilianzishwa na watu wamechangia zaidi ya dola 30,000 ili kumsaidia mtoto huyo kwenda kupata mafunzo katika akademia maarufu ya FC Barcelona (La Masia) nchini Uhispania.