Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa mechi zilizozalisha mabao mengi Kombe la dunia la klabu

KAMBA Pict
KAMBA Pict

Muktasari:

  • Ingawa baadhi ya mechi huwa ni ngumu kuzalisha mabao, kuna mechi nyingine  hugeuka kuwa shoo za mabao kutokana na idadi kubwa ya mabao yanayofungwa.

FLORIDA, MAREKANI: KATIKA historia ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu, mabao yamekuwa si tu njia ya ushindi bali pia burudani halisi kwa mashabiki duniani kote.

Ingawa baadhi ya mechi huwa ni ngumu kuzalisha mabao, kuna mechi nyingine  hugeuka kuwa shoo za mabao kutokana na idadi kubwa ya mabao yanayofungwa.

Wikiendi iliyopita iliwekwa historia nyingine pale mechi kati ya Bayern Munich na Auckland City ilipozalisha mabao mengi zaidi katika historia ya michuano hiyo. Pamoja na mchezo huo hapa tumekuwekea mechi saba zilizowahi kuzalisha mabao mengi zaidi katika historia ya michuano hii.


07. Barcelona vs Santos

Mabao: 4

Desemba, 18, 2011 - Japan

Hii ni fainali nyingine ambayo ilizalisha mabao mengi. Barca ambayo ilikuwa chini ya Pep Guardiola kwa wakati huo mabao yake yalifungwa na Lionel Messi aliyetupia kambani mara mbili kisha Xavi Hernandes na Cesc Fabregas wakahitimisha ushindi wa kihistoria kwa kufunga bao moja kila mmoja.


06. Real Madrid vs Kashima Antlers

Mabao: 6

Desemba, 18, 2016 - Japan

Fainali (Muda wa Ziada)

Kwenye fainali hii ya kusisimua, Cristiano Ronaldo ndio aliibuka shujaa baada ya kufunga hat-trick na kuiwezesha Real Madrid kushinda mabao 4-2 katika muda wa dakika 30 za ziada baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Ronaldo alifunga bao la tatu kwa Madrid na la pili kwake katika dakika ya 98, kisha akafuta kabisa matumaini ya Kashima katika dakika ya 104.


5. Monterrey vs Al Ahly

Mabao: 6

Desemba, 16, 2012- Japan

Mchezo huu ambao ulikuwa wa kuwania nafasi ya tatu uliopigwa kwenye dimba la Nissan, jijini Yokohama ulizikutanisha Ahly na Monterrey ambazo zilikuwa na maumivu ya kujeruhiwa kwenye hatua ya nusu fainali.

Ahly ilikuwa imepoteza mbele ya Corinthians ya Brazil wakati Monterrey ikichapwa na Chelsea.

Kwenye mechi hiyo mabao mawili ya Monterrey yalifungwa na Cesar Delgado kisha  Jesus Corona, Leobardo Lopez na Hiram Mier wakafunga bao moja moja wakati bao pekee la Ahly likifungwa na Mohamed Aboutrika katika dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha pili.


4. Al Hilal vs Al Jazira

Mabao: 7

Februari, 06, 2022 – UAE

Robo Fainali

Al Hilal ilipata nafasi ya kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuitandika Al Jazira kwa mabao 6-1. Huu ndio ushindi mkubwa zaidi kwa timu hii kuwahi kuupata katika michuano hii.

Mabao sita yote yalifungwa na wachezaji sita tofauti ambapo Odion Ighalo (aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Manchester United) alitupia pamoja na Matheus Pereira, Mohammed Kanno, Salem Al-Dawsari, Moussa Marega na Andre Carrillo.

Bao la kufutia machozi la Al Jazira lilifungwa na Abdoulay Diaby.


3. Real Madrid vs Al Hilal

Mabao: 8

Februari, 11, 2023 -

Morocco

Fainali

Real Madrid iliibuka mabingwa baada ya kuishinda Al Hilal ya Saudi Arabia kwa 5-3 katika mchezo ambao hadi leo unashikilia rekodi ya kuwa fainali iliyozalisha mabao mengi zaidi kwenye historia ya michuano hii.

Mabao ya Madrid katika mechi hii yalifungwa na Vinicius Jr (2) sawa na Federico Valverde wakati Benzema akifunga moja.

Al-Hilal wafungaji wao walikuwa ni Moussa Marega na Luciano Vietto.


2. Esperance vs Al Sadd

Mabao: 8

Desemba 17, 2019 - Qatar

Esperance ya Tunisia ilipata ushindi mkubwa dhidi ya Al Sadd ya Qatar. Mabao ya haraka na mashambulizi ya nguvu yaliifanya mechi hii kuzalisha mabao manane.

Mabao ya Esperance yalifungwa na Hamdou Elhouni aliyepiga hat-trick, pia Anice Badri alifunga mawili na Sameh Derbali akafunga moja.

Kwa upande wa Al Sadd mabao yao mawili ya kufutia machozi yalifungwa na Boualem Khoukhi na Hassan Al-Haydos.


1.  Bayern Munich vs Auckland City

Mabao: 10

Juni 15, 2025 - Marekani

Hatua ya Raundi ya Kwanza

Mchezo huu ambao ulipigwa Jumapili ya wikiendi iliyopita na Bayern Munich kuibuka na ushindi wa mabao 10-0 dhidi ya Auckland City, uliweka rekodi ya kuwa mechi ya kwanza kuzalisha mabao mengi zaidi katika historia ya michuano hiyo.

Katika mchezo huo, Musiala alifunga hat-trick, wakati Muller, Coman na Olise wakifunga mara mbili kisha bao la 10 likatupiwa wavuni na Sacha Boey.

Bayern walitawala mchezo huu kutoka mwanzo hadi mwisho, huku Auckland City wakikosa hata shuti moja lililolenga lango.