Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hakuna namna ni Harry Kane tu!

KANE Pict

Muktasari:

  • Kinachoelezwa ni kwamba, straika Harry Kane amewekwa namba moja na mabosi wa Barcelona katika mpango wao wa kusaka straika mpya na mchakato wa kunasa huduma yake, unaweza kufanyika kwenye dirisha la uhamisho lijalo la majira ya kiangazi.

BARCELONA, HISPANIA: CHUMA kimoja kikitoka, kingine kinaingia. Hicho ndicho kinachopangwa kufanyika huko Barcelona katika msako wa kusaka straika mpya wa kucheza kwenye fowadi yao msimu ujao.

Kinachoelezwa ni kwamba, straika Harry Kane amewekwa namba moja na mabosi wa Barcelona katika mpango wao wa kusaka straika mpya na mchakato wa kunasa huduma yake, unaweza kufanyika kwenye dirisha la uhamisho lijalo la majira ya kiangazi.

Kane, 32, alikuwa na kiwango bora kabisa katika msimu wake wa kwanza huko Bayern Munich na anaendelea kuonyesha makali ya maana, akifunga mabao 23 katika mechi 17.

KAN 01

Kiwango chake bora kwenye kutupia nyavuni kimefanya klabu nyingi vigogo vya Ulaya kusaka huduma yake na ndio maana Barcelona ipo kwenye harakati za kunasa saini yake.

Tottenham Hotspur ilibainisha dhamira yake ya kumrudisha straika huyo wa zamani kwenye kikosi chao baada ya kumuuza miaka miwili iliyopita kwa ada ya Pauni 104 milioni.

Lakini, kwa mujibu wa Mundo Deportivo, ripoti zinasisitiza kwamba Barcelona ndiko mahali ambako Kane anaonekana wazi atakwenda kukipiga huko kuanzia msimu ujao.

KAN 02

Mabosi wakubwa wa klabu hiyo ya Nou Camp kwa sasa wanakuna vichwa juu ya kusaka huduma ya straika mpya mwenye viwango vya dunia kutokana na mkali aliyepo kwenye kikosi chao kwa sasa, Robert Lewandowski kutarajia kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Lewandowski kwa sasa umri wake ni miaka 37 na mkataba wake huko Barca utafika tamati Juni mwakani, licha ya kwamba kuna kipengele kinachowaruhusu mabosi wa timu hiyo ya Catalunya kumwongezea mkataba wa mwaka mmoja ili kubaki kwenye kikosi hicho hadi 2027.

Na katika mchakato huo wa kujadili hatima ya Lewandowski kwenye kikosi cha Barca kama ataondoka au kubaki, ndipo jina la Kane linapoibuka kwenye mjadala, ambapo rais wa klabu hiyo, Joan Laporta amemweka kwenye mipango yake supastaa huyo wa England.

Mkataba wa nahodha huyo wa England, Kane huko Bayern Munich umeripotiwa kuwa na kipengele kinachotajwa bei yake anayouzwa kuwa ni Pauni 57 milioni na kitaanza kufanya kazi kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

KANE Pict

Hata hivyo, kwenye kunasa saini ya Kane, Barcelona itakuwa na kasheshe kubwa la kuchuana kutokana na timu nyingine kuhitaji huduma yake. Na kama Kane itakuwa ngumu kumpata, Barcelona imeweka mtego pia kwa straika wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, licha ya kwamba timu yake haionekani kama itakubali kirahisi kumwachia Muargentina huyo aondoke.

Fowadi huyo wa zamani wa Manchester City mkataba wake huko Atletico umebakiza miaka minne. Kwenye La Liga, Barca kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo, pointi tatu nyuma ya vinara Real Madrid na Jumamosi itakipiga na Athletic Bilbao.