Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fulham, Barcelona zamwinda Heaven

Muktasari:

  • Heaven, mwenye umri wa miaka 20, amekuwa akipitia kipindi kigumu tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa United, Ruben Amorim, ambaye alimpa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

MANCHERSTER, ENGLAND: BEKI wa Manchester United, Ayden Heaven, anafikiria kuondoka kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili la Januari, kufuatia kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu.

Heaven, mwenye umri wa miaka 20, amekuwa akipitia kipindi kigumu tangu kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa United, Ruben Amorim, ambaye alimpa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Hata hivyo, ujio wa makocha waliofuata umebadili hali yake ndani ya kikosi hicho, huku akishindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Kocha mpya wa United, Mauricio Pochettino, katika mchezo wake wa kwanza wa kusimamia timu hiyo dhidi ya Liverpool Uwanja wa Anfield, aliamua kuwatumia Matthijs de Ligt na Leny Yoro katika safu ya ulinzi.

Hata hivyo, Yoro alidumu uwanjani kwa dakika nane pekee kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Katika hatua hiyo, Harry Maguire aliingizwa kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi, huku Heaven akibaki benchi bila kucheza.

Beki huyo wa England chini ya miaka 20 alijiunga na Manchester United akitokea Arsenal Februari 2025, lakini kwa sasa anapitia kipindi cha kuwa chini ya makocha watatu tofauti tangu awasili Old Trafford.

Taarifa zinaeleza kuwa klabu za Fulham na Barcelona zimeonyesha nia ya kumsajili beki huyo wa kati katika dirisha lijalo la usajili.

Fulham pia imehusishwa na uwezekano wa kumwachia beki wake Calvin Bassey kujiunga na Manchester United, ingawa mpango huo unaonekana kuwa mgumu kutimia kutokana na umuhimu wa Bassey katika kikosi cha The Cottagers.

Kwa upande wa Heaven, inaelezwa kuwa chaguo lake la kwanza ni kuondoka kwa mkopo ili kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara na kuendeleza kiwango chake, ingawa hatakuwa na tatizo kufikiria ofa nzuri ya uhamisho wa moja kwa moja.

Mara ya mwisho Heaven kuanza katika kikosi cha kwanza cha United kwenye Ligi Kuu England ilikuwa mwishoni mwa Oktoba, katika kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Bournemouth, kabla ya kutolewa dakika ya 65.

Pia, hajamaliza dakika zote 90 katika mchezo wowote wa United tangu katikati ya Septemba, alipocheza katika kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Brighton kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Wakati huohuo, Pochettino anatarajiwa kuimarisha safu yake ya ulinzi katika dirisha la Januari, huku akitajwa kuhitaji wachezaji wenye uzoefu zaidi ili kujaribu kuinusuru timu hiyo dhidi ya hatari ya kushuka daraja.

United inadaiwa kuwa katika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kabla ya mchezo wake dhidi ya Brentford Jumamosi.

Kwa sasa, kikosi cha Pochettino kinaendelea kutafuta namna ya kurejesha makali yake baada ya mwenendo usioridhisha wa matokeo, kikiwa na kibarua kingine dhidi ya Sporting Lisbon katika mchezo wa usiku wa leo.