Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Flick asema tena kuhusu Marcus Rashford

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Rashford alifikisha jumla ya mabao matano na asisti tano katika mechi 12 alizoichezea Barca msimu huu, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Olympiakos katika Ligi ya Mabingwa wiki hii.

BARCELONA, HISPANIA: KOCHA wa Barcelona, Hans Flick amesisitiza Marcus Rashford ni mchezaji muhimu sana katika mipango yake na siku hadi siku atazidi kuimarika na kuwa bora zaidi.

Rashford alifikisha jumla ya mabao matano na asisti tano katika mechi 12 alizoichezea Barca msimu huu, baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Olympiakos katika Ligi ya Mabingwa wiki hii.

Staa huyu ambaye amejiunga Barca kwa mkopo kutoka Manchester United alichezeshwa kama mshambuliaji wa kati na Flick, ambaye alikuwa anamkosa straika wake Robert Lewandowski anayesumbuliwa na majeraha.

RASH 01

Vilevile, Flick aliamua kumweka benchi Ferran Torres ambaye angeweza kucheza eneo hilo na badala yake akaamua kumtumia  Rashford ambaye tangu atue ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuchezeshwa katika nafasi hiyo.

Ingawa fundi huyu yuko kwa mkopo hadi mwishoni wa msimu huu, ripoti zinadai Flick amewaambia mabosi wa Barca wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha wanambakisha.

Katika mkataba wake kuna kipengele kinachoiwezesha Barcelona kumnunua mazima kwa kutoa Euro 30 milioni.

Akizungumza kuhusu kiwango cha Rashford na mchango wake katika timu  Flick amesema: "Kwangu mimi, Rashford anafanya vizuri sana na ni mchezaji muhimu kwa timu. Ana kasi sana, anashirikiana vizuri na wenzake  na kadri anavyopata kujiamini, ndivyo anavyokuwa muhimu zaidi katika timu."

RASH 02

Kwa miaka ya karibuni Rashford amekuwa akicheza zaidi upande wa kushoto, lakini Jumanne alipewa nafasi ya kucheza kama mshambuliaji wa kati, huku Lamine Yamal akicheza upande wa kulia, Fermin Lopez akawa namba 10 na kijana Dro Fernandez akacheza upande wa kushoto.

Barcelona kwa sasa iko nafasi ya pili kwenye La Liga, pointi mbili nyuma ya Real Madrid na katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, iko nafasi ya tisa baada ya kushinda michezo miwili na kupoteza mmoja. Jumapili ya wiki hii itakutana na Real Madrid katika El Clasico kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.

Flick alipoulizwa kuhusu mechi hiyo amesema licha yakuwa hawajashinda hata mechi moja ya El Classico kati ya nne zilizopita, hiyo inabaki kuwa tu ni historia na sasa wataingia kivingine na ana matumaini watashinda.