Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ferdinand amaliza utata wa nani bora kati ya Rice na Caicedo

RIO Pict

Muktasari:

  • Ferdinand ambaye aliitumikia Man United kwa mafanikio ameeleza msimamo wake kwenye mjadala huo, akisema kuwa wachezaji hao wana sifa zinazofanana, lakini pia kila mmoja ana umahiri wa kipekee.

Gwiji wa soka nchini England, Rio Ferdinand ametoa maoni yake kuhusu nani bora kati ya nyota wa Arsenal, Declan Rice na Moisés Caicedo wa Chelsea, ambao wameibua mijadala mitandaoni kufuatia kuonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu 2025-2026.

Ferdinand ambaye aliitumikia Man United kwa mafanikio ameeleza msimamo wake kwenye mjadala huo, akisema kuwa wachezaji hao wana sifa zinazofanana, lakini pia kila mmoja ana umahiri wa kipekee.

Amesema anaamini uchaguzi wa mchezaji unategemea ni nafasi gani anacheza uwanjani, lakini kwa wawili hao inakuwa kazi ngumu kusema nani ni bora kuliko mwenzake.

RI 03

Hata hivyo Ferdinand amekiri kuwa, Rice ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya mbele zaidi, huku Caicedo akiwa na uwezo mkubwa wa kukatisha mashambulizi ya timu pinzani.

Akizungumza katika kipindi chake cha Rio Ferdinand Presents, amesema: "Nadhani wana ufanano mkubwa kwenye uchezaji wao. Declan, ukimpa uhuru wa kwenda mbele, atakupa mchango mkubwa kwenye mashambulizi. Lakini Caicedo, kwa upande wa ulinzi, anasoma hatari mapema na kwa ufanisi zaidi, hiyo ndiyo silaha yake kuu. 

RI 02

"Kwa kweli hakuna tofauti kubwa sana kati yao kwa sasa. Ningefurahia kuwa na mmoja wao. Wote wawili walipokuwa sokoni, nilikuwa naihimiza Manchester United kuwasajili hawa jamaa."

Ferdinand ameongeza kuwa, hawezi kuacha kufikiria jinsi mmoja wao angeweza kuwa na athari kubwa kwa Manchester United, iwapo klabu hiyo ingemsajili.

RI 01

"Niliona thamani ya Caicedo. Niliamini angekuwa mchezaji wa kipekee kwa Manchester United. Vivyo hivyo na Declan angekuwa usajili wa ajabu. Inategemea unataka wacheze wapi. Kama unahitaji kiungo mkabaji, ningesema Caicedo. Lakini kama unamchezesha kama namba 8, ningemchagua Declan. Ukimruhusu Declan kwenda mbele, atakufungia magoli zaidi kuliko Caicedo," amesema.