Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rio kicheko kipa Onana kuondoka

RIO Pict

Muktasari:

  • Onana anaondoka Man United kwa mkopo wa msimu mzima kwenda Uturuki kwenye klabu ya Trabzonspor baada ya ujio wa kipa mpya, Senne Lammens kikosini Old Trafford.

MANCHESTER, ENGLAND: BEKI wa zamani, Rio Ferdinand amefurahia kitendo cha Manchester United kumfungulia mlango wa kutokea kipa Andre Onana akidai msimu uliompita alimweka kwenye wakati mgumu sana.

Onana anaondoka Man United kwa mkopo wa msimu mzima kwenda Uturuki kwenye klabu ya Trabzonspor baada ya ujio wa kipa mpya, Senne Lammens kikosini Old Trafford.

Onana amekuwa chaguo la kwanza tangu alipotua Old Trafford akitokea Inter Milan mwaka 2023. Lakini, kiwango chake kibovu kimemshuhudia Altay Bayindir akichukua nafasi ya kuwa kipa namba moja msimu huu kabla ya ujio wa Lammens kwa ada ya Pauni 18 milioni akitokea Royal Antwerp kwenye siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi.

Kipa huyo wa zamani wa Ajax, Onana, ambaye alisajiliwa na Erik ten Hag, alipokuwa Man United, amekubali kwenda kwa mkopo Trabzonspor kwa ajili ya msimu wa 2025/26.

Man United haitalipwa ada yoyote ya mkopo na klabu hiyo ya Uturuki haitamchukua jumla kipa huyo wa kimataifa wa Cameroon.

Lakini, Ferdinand alionekana kufurahishwa na kitendo tu cha Onana kuondoka kwenye timu msimu huu, akisema: “Nadhani Omar Berrada, anayesimamia oparesheni za soka kwenye klabu, ameonyesha wazi hawezi kuendelea kubaki na wachezaji ambao hawana tena maana ya kuwapo kwenye klabu.

“Hawezi kuwa na mchezaji ambaye hana uwezo, hachezji vizuri na si mtu sahihi kuwa kwenye timu. Hawezi kuwa na mchezaji ambaye haleti kitu cha maana kwenye timu. Nadhani sasa, tunaanza kuona hii inavyoelekea kuwa klabu ya mpira.

“Tulilazimika kuwa na wachezaji kwa sababu ya hali mbaya ya kiuchumi na tukabaki kuwa nao, kuendelea kutaabika.”

Kocha Ruben Amorim aliingia kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka huu akiwa na orodha ya wachezaji ambao aliwaambia wazi watafute sehemu ya kwenda kwa sababu hawapo kwenye mipango yao, akiwamo Marcus Rashford, Jadon Sancho, Antony, Alejandro Garnacho na Tyrell Malacia. Karibu wachezaji wote hao, isipokuwa Mallacia wameshaondoka, huku wengine waliofunguliwa mlango wa kutokea ni Rasmus Hojlund, Victor Lindelof na Christian Eriksen.