Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fenerbahce yatikiswa, kocha ajiuzulu

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Kartal, ambaye aliteuliwa kuinoa Fenerbahce mwezi Juni, alitoa taarifa hiyo kwa kushtukiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, akisema ameamua kuondoka kwa masilahi ya klabu.

ISTANBUL, UTURUKI: FENERBAHCE imeingia kwenye sintofahamu baada ya kocha wake Ismail Kartal kutangaza kujiuzulu mara baada ya timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya AS Roma katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Alhamisi usiku.

Kartal, ambaye aliteuliwa kuinoa Fenerbahce mwezi Juni, alitoa taarifa hiyo kwa kushtukiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, akisema ameamua kuondoka kwa masilahi ya klabu.

Kocha huyo amesema amekuwa na kipindi kizuri tangu alipokabidhiwa timu hiyo, huku akiwapongeza viongozi wa klabu kwa ushirikiano wao pamoja na wachezaji kwa namna walivyofanya kazi tangu maandalizi ya msimu yalipoanza.

“Nimekuwa hapa kwa miezi mitatu sasa. Tangu mwanzo wa msimu tumekuwa tukifanya mazoezi pamoja na wachezaji na kumaliza kambi za maandalizi. Mwenyekiti wetu na bodi wamejaribu kutusaidia kwa kila kitu. Zilikuwa siku nzuri,” amesema Kartal.

KOCH 01

Hata hivyo, baada ya kutoa kauli hiyo, Kartal aliwashangaza wengi kwa kutangaza kwamba mchezo dhidi ya Roma ulikuwa wa mwisho kwake akiwa kocha wa Fenerbahce.

“Usiku wa leo nawapongeza wachezaji wangu na najiuzulu. Napenda kuwashukuru mashabiki wetu, waandishi wa habari, benchi langu la ufundi na wachezaji wangu kwa sapoti yote niliyoipata hadi sasa,” amesema.

Kartal amesisitiza uamuzi wake haukutokana na kutoridhishwa na wachezaji, bali aliamua kuondoka mapema ili kuipa klabu nafasi ya kuendelea na mipango yake bila yeye.

“Nimefanya uamuzi huu ili kuipa klabu yangu nafasi. Tumeufanya uamuzi huu kama timu. Nataka kuisaidia Fenerbahce, wachezaji wangu na makocha watakaokuja hapa baadaye. Ndiyo sababu naondoka sasa, wakati bado ni mapema,” amesema.

KOCH 02

Hata hivyo, mwenyekiti wa Fenerbahce, Aziz Yildirim, alipinga mara moja taarifa hiyo na kusema klabu haijakubali kujiuzulu kwa Kartal.

“Bado ni kocha wetu na nimemwambia hivyo pia. Tutaendelea pamoja, sisi ni kama familia. Hadi nitakapoondoka, yeye atabaki kuwa kocha mkuu,” amesema Yildirim.

Jambo lililoongeza mshangao ni kwamba hata baadhi ya wachezaji hawakuwa na taarifa kuhusu uamuzi huo.

KOCH 03

Beki wa kushoto Archie Brown alionekana kushangazwa alipoambiwa kuhusu kujiuzulu kwa Kartal.

Hivyo, licha ya kocha huyo kutangaza kuondoka, kauli ya mwenyekiti imeacha mustakabali wake ukiwa haujaeleweka.