Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Enzo Fernandez aingia anga za Real Madrid

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Taarifa za ndani kutoka Madrid zinadai staa huyu anaonekana kuwa sehemu ya mpango wa muda mrefu wa timu na anaweza kuvaa viatu vya viungo wakubwa waliopita kama Luka Modric na Toni Kroos.

KIUNGO wa kati wa Chelsea, Enzo Fernandez, 24, anatajwa kuwa kwenye rada za Real Madrid inayotaka kumsajili mwisho wa msimu huu.

Taarifa za ndani kutoka Madrid zinadai staa huyu anaonekana kuwa sehemu ya mpango wa muda mrefu wa timu na anaweza kuvaa viatu vya viungo wakubwa waliopita kama Luka Modric na Toni Kroos.

Hata hivyo, Chelsea wameweka wazi kuwa staa huyu hatouzwa kwa kiasi cha chini ya Pauni 120 milioni ambacho kinatajwa kuwa kikwazo cha dili hilo kwa sasa.

Fernandez, ambaye alishinda Kombe la Dunia mwaka 2022 akiwa na timu ya taifa ya Argentina, ameendelea kuwa kiungo tegemeo katika kikosi cha Chelsea chini ya Enzo Maresca na anadaiwa kutamani sana kutua Madrid lakini hataki kulazimisha dili hilo badala yake anataka timu zikubaliane.

Msimu huu, Enzo ana wastani wa asilimia 91 ya pasi sahihi kwa kila mchezo, akifunga mabao manne  na kutoa asisti sita za mabao katika mashindano yote.

Mkataba wa fundi huyu na Chelsea unatarajiwa kumalizika mwaka 2032 na msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote.


Adam Wharton

KIUNGO wa Crystal Palace, Adam Wharton mwenye umri wa miaka 21, anaripotiwa kuwa katika rada za Manchester United kuelekea dirisha lijalo la usajili.

Wharton, ambaye amekuwa mchezaji muhimu kwa Palace tangu ajiunge nao akitokea Blackburn Rovers mwaka 2024, pia amekuwa katika rada za timu nyingine kubwa za Ulaya. Man United ipo tayari kutoa hadi Pauni 60 milioni ili kumpata.


Morten Hjulmand

TOVUTI ya Fichajes ya Hispania imefichua kwamba Manchester United na Tottenham zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon, Morten Hjulmand, mwenye umri wa 26. Hjulmand, ambaye ni raia wa Denmark, amekuwa mchezaji muhimu katika mfumo wa kocha Ruben Amorim huko Sporting, akicheza mechi 39 msimu uliopita na kusaidia klabu hiyo kushinda taji la Ligi Kuu ya Ureno.

Sporting inataka ada ya takriban Euro 45 milioni ili kumwachia staa huyo ambaye Man United inamwona kama mbadala sahihi wa Casemiro.


Dayot Upamecano

BAYERN Munich bado ina mpango wa kumuongeza mkataba beki wake kisiki raia wa Ufaransa, Dayot Upamecano mwenye umri wa miaka 26, licha ya mazungumzo kuonekana kuwa magumu hadi sasa.

Staa huyu anadaiwa kutaka kuondoka mwisho wa msimu huu na timu inayopewa nafasi kubwa ya kumpata ni Liverpool. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu na vigogo wamevutiwa na hilo.


Max Kilman

CRYSTAL Palace inamwangalia beki wa West Ham United, Max Kilman, 28, kama chaguo sahihi la kuchukua nafasi ya Marc Guehi ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na anaweza akauzwa Januari mwakani.

Kwa mujibu wa tovuti ya Football Insider, Palace inajiandaa kupokea ofa kutoka kwa vigogo kama Liverpool, Chelsea na Manchester United wanaomtaka Guehi.

Kilman, aliwahi kuwa nahodha wa Wolves kabla ya kujiunga na West Ham kwa Pauni 35 milioni, msimu uliopita.


Tyrell Malacia

GALATASARAY ya Uturuki inatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kushinda vita ya kumsajili beki wa kushoto wa Manchester United, Tyrell Malacia, 26, katika dirisha lijalo. Malacia hajacheza mechi yoyote United tangu msimu uliopita kutokana na jeraha sugu la goti lililohitaji afanyiwe upasuaji mara mbili. Kocha Ruben Amorim anataka kumruhusu aondoke ili akapate nafasi ya kucheza kabla ya kumrudisha.


Joshua Zirkzee

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Joshua Zirkzee, 24, anatajwa kuwindwa sana na AS Roma kuelekea dirisha lijalo la majira ya baridi.

Zirkzee, ambaye hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man United tangu kuanza kwa msimu huu anaweza akatua Roma kwa mkataba wa mkopo ambao utakuwa na kipengele cha kumnunua mazima mwisho wa msimu.

Mkataba wake na Man United unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Harry Maguire

BEKI wa Manchester United, Harry Maguire, 32,  anaripotiwa kukataa ofa ya takribani Pauni 500,000 kwa wiki kutoka Saudi Arabia na badala yake amekubali kupunguza mshahara wake ili kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mashetani wekundu.

Licha ya kupoteza nafasi yake kama nahodha wa timu hiyo msimu uliopita, Maguire ameonekana kuendelea kuwa katika mipango ya kocha Ruben Amorim.

Inaelezwa moja ya sababu zilizofanya beki huyu akatae ofa hiyo ni kutaka kucheza soka la kiushindani ili kuitwa katika Kombe la Dunia mwakani.