Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Napoli sasa yamuomba Kobbie Mainoo kwa mkopo

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Manchester United hali inayosababisha afikirie kuondoka. Awali, alijaribu kuondoka katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana baada ya Man United kugoma kumuuza.

NAPOLI imewasilisha rasmi maombi kwenda Manchester United kwa ajili ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Kobbie Mainoo, katika dirisha la usajili la Januari.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Manchester United hali inayosababisha afikirie kuondoka. Awali, alijaribu kuondoka katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana baada ya Man United kugoma kumuuza.

Hata hivyo, licha ya kumbakisha, Mainoo bado haonekani kuwa na nafasi katika kikosi hicho chini ya Ruben Amorim ambaye amekuwa akieleza kwamba kiungo huyu anatakiwa kubadilika na kufuata anachomwambia ili amchezeshe.

Mkataba wa kinda huyu unamalizika 2027 na mabosi wa United wameendelea kushikilia msimamo wa kuhitaji ada inayofikia Pauni 40 milioni ambayo inaonekana kuwa kubwa kwa timu nyingi.


Kalvin Phillips

EVERTON inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya England, Kalvin Phillips, 29, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Phillips ni miongoni mwa wachezaji ambao hawapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Man City, hali iliyosababisha aombe kuondoka mwisho wa msimu huu.  Mkataba wa sasa wa staa huyo Man City unamalizika 2027.


Michail Antonio

BRENTFORD haina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Jamaica,  Michail Antonio, 35, licha ya kwamba amekuwa akifanya mazoezi na timu hiyo ya Ligi Kuu England. Antonio aliachana na West Ham mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya saba. Alikosa mechi nyingi za msimu uliopita kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali ya gari ambayo alinusurika kifo.



Harry Maguire

MANCHESTER United inaendelea kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Harry Maguire, 32, kuhusu mkataba mpya, na tayari vikao vya ana kwa ana vimefanyika. Maguire ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu, anataka kubakia Man United na yupo tayari pia kupunguza hadi mshahara wake ili kuhakikisha suala la mkataba mpya linafanikiwa.


Kenan Yildiz

MANCHESTER United ipo tayari kutoa Pauni 78 milioni kwenda Juventus ili kuipata saini ya mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Uturuki, Kenan Yildiz, 20, ambaye pia anawindwa na Chelsea. Yildiz ameonyesha kiwango cha juu akiwa na Juventus na amekuwa gumzo kwa kuwa na uwezo wa kucheza kama namba 10 na tisa. Huduma ya staa huyu pia inawindwa na Liverpool.


Carlos Baleba

MANCHESTER United ina kipaumbele cha kusajili kiungo katika dirisha lijalo na miongoni mwa mastaa ambao imewaweka katika rada zake ni Carlos Baleba, 21, wa Brighton na timu ya taifa ya Cameroon, pamoja na Elliot Anderson, 22, raia wa England anayechezea Nottingham Forest. Baleba amekuwa na msimu mzuri Brighton tangu ajiunge nao akitokea Lille sawa na ilivyo kwa Anderson.


Marc Guehi

CRYSTAL Palace inajiandaa kusikiliza ofa kutoka timu zinazomhitaji beki wake raia wa England, Marc Guehi, katika dirisha la usajili la Januari  ambapo imepanga kumuuza ili asiondoke bure katika dirisha la majira ya kiangazi mwakani. Liverpool, Barcelona na Real Madrid ni kati ya timu ambazo zinadaiwa kuendelea kuonyesha nia ya kumsajili staa huyu mwenye umri wa miaka 25.


Murillo Santiago

BEKI wa kati wa Nottingham Forest na timu ya taifa ya Brazil mwenye umri wa miaka 23, Murillo Santiago ni mmoja wa wachezaji walioko katika kurasa za kwanza kwenye orodha ya mastaa ambao Chelsea inataka kuwasajili Januari ili kuimarisha safu yao ya ulinzi. Murillo ameonyesha kiwango bora tangu ajiunge na Nottingham na mbali ya Chelsea timu kuwa nyingi pia zinaitamani huduma yake.