Enzo amsukuma mwamuzi aokoa kadi nyekundu
Muktasari:
- City ilipoteza mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Etihad baada ya mabingwa hao watetezi wa Ulaya, PSG kuonyesha ubora mkubwa, wakipata mabao matatu kipindi cha kwanza kupitia Desire Doue, Ousmane Dembele na Vitinha.
LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa soka wamehoji kwa nini kiungo Enzo Fernandez, hakutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumgonga mwamuzi katika kipigo cha mabao 4-2 ilichopata Manchester City dhidi ya Paris Saint-Germain (PSG)katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
City ilipoteza mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Etihad baada ya mabingwa hao watetezi wa Ulaya, PSG kuonyesha ubora mkubwa, wakipata mabao matatu kipindi cha kwanza kupitia Desire Doue, Ousmane Dembele na Vitinha.
Mshambuliaji wa City, Erling Haaland alifunga mabao mawili huku Maghnes Akliouche akiongeza bao jingine kwa PSG, na kuzima matumaini ya City ya kurejea mchezoni.
Hata hivyo, tukio lililozua mjadala lilikuwa la Fernandez kugongana na mwamuzi Sven Jablonski, ambaye alionekana kuanguka baada ya kiungo huyo wa Argentina kumsukuma mgongoni kwa mikono yote miwili.
Fernandez alikuwa akikimbilia mpira, lakini njia yake ikazuiwa na mwamuzi huyo kutoka Ujerumani. Badala ya kubadili mwelekeo, kiungo huyo aliendelea na safari yake na kugongana na Jablonski kwa nyuma.
Marudio ya video yalionyesha Fernandez akiweka mikono yake miwili mgongoni mwa mwamuzi na kuisukuma kwa mbele, hali iliyomfanya Jablonski aanguke chini. Mwamuzi huyo alionekana kushangazwa na tukio hilo alipogeuka kuangalia kilichotokea.
Fernandez hakufuatilia mpira uliokuwa umeachia, badala yake alisimama uwanjani huku mpira ukipita mbele yake.
Tukio hilo liliwaacha mashabiki wakishangaa kwa nini kiungo huyo wa zamani wa Chelsea hakuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Shabiki mmoja aliandika: “Enzo Fernandez alimsukuma mwamuzi!”
Mwingine amesema: “Kwa kweli, Enzo Fernandez alimchezea mwamuzi faulo kwa kuzuia njia yake.”
Shabiki wa tatu alihoji: “Kwa nini Enzo hakupata kadi nyekundu kwa tukio hilo dhidi ya mwamuzi?”
Naye shabiki mwingine alisisitiza: “Hiyo ni kadi nyekundu ya wazi kwa Enzo.”