Droo robo fainali CAF ni kivumbi na jasho
Muktasari:
- Sherehe za upangaji huo wa droo ya robo fainali iliyofanyika Cairo, Misri mchana wa Jumanne, ulihusishwa pia nane bora ya Kombe la Shirikisho la Afrika. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mabingwa watetezi Pyramids FC wamepangwa kukutana na FAR ya Morocco, huku timu hiyo ya Jeshi la Kifalme ikitarajia kuvuruga ndoto za klabu ya Cairo kutwaa taji la pili mfululizo.
CAIRO, MISRI: MAMBO ni moto. Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limefanya droo ya robo fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika huku likizipanga Esperance de Tunis na Al Ahly kumenyana kwenye hatua hiyo ya nane bora.
Sherehe za upangaji huo wa droo ya robo fainali iliyofanyika Cairo, Misri mchana wa Jumanne, ulihusishwa pia nane bora ya Kombe la Shirikisho la Afrika. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, mabingwa watetezi Pyramids FC wamepangwa kukutana na FAR ya Morocco, huku timu hiyo ya Jeshi la Kifalme ikitarajia kuvuruga ndoto za klabu ya Cairo kutwaa taji la pili mfululizo.
Mabingwa mara 12, Al Ahly, watarejesha upinzani wao wa kihistoria dhidi ya Esperance de Tunis wakati mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho, RS Berkane watapimana nguvu na Al Hilal ya Sudan ambayo ipo kwenye kiwango bora.
Washindi wa pili msimu uliopita, Mamelodi Sundowns watavaana na Stade Malien katika pambano la Kusini dhidi ya Magharibi mwa Afrika.
Kwa upande wa nusu fainali, washindi wa mechi za Esperance dhidi ya Al Ahly na Sundowns dhidi ya Stade Malien wapo upande mmoja wa droo, huku washindi wa ASFAR dhidi ya Pyramids na Berkane dhidi ya Al Hilal wakiwa upande mwingine.
Katika Kombe la Shirikisho Afrika, mabingwa mara mbili Zamalek SC wamepangwa kukutana na AS Otoho ya Congo.
Wakati huo huo, AS Maniema Union ya DR Congo itajaribu kuishangaza USM Alger ya Algeria katika moja ya mechi inayotazamiwa kuwa na upinzani mkali, huku klabu za Morocco, OC Safi na Wydad Casablanca, vitakutana katika pambano la ndani ya ligi ya Botola Pro, huku Al Masry ya Misri na CR Belouizdad wakikabiliana katika dabi ya Afrika Kaskazini.
Kwa njia ya nusu fainali, washindi wa mechi za Maniema dhidi ya USMA na Safi dhidi ya Wydad watakutana hatua ya nne bora, huku washindi wa Masry dhidi ya CRB na Otoho dhidi ya Zamalek wakiwa upande mwingine wa droo.
Robo fainali za mashindano yote mawili zinatarajiwa kuanza kwa mechi za mkondo wa kwanza kati ya Machi 13–15, huku mechi za marudiano zikipangwa kufanyika kati ya Machi 20–22.
DROO KAMILI YA CAF
Kombe la Shirikisho Afrika
Al Masry vs CR Belouizdad
AS Otoho vs Zamalek SC
OC Safi vs Wydad Casablanca
AS Maniema Union vs USM Alger
Ligi ya Mabingwa Afrika
Esperance de Tunis vs Al Ahly
Mamelodi Sundowns vs Stade Malien
ASFAR vs Pyramids FC
RS Berkane vs Al Hilal.