Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la fundi Ugarte kalishika McTominay

Muktasari:

  • Man United inatafuta pesa kwa ajili ya kunasa saini ya kiungo wa Paris Saint-Germain, Manuel Ugarte

MANCHESTER, ENGLAND: NDO hivyo. Ishu ya Scott McTominay kuuzwa bado ipo kwenye utata mkubwa kwa kipindi hiki ambacho Manchester United inataka kuboresha safu yake ya kiungo klabu ya dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi huko Ulaya kufungwa, Agosti 30.

Man United inatafuta pesa kwa ajili ya kunasa saini ya kiungo wa Paris Saint-Germain, Manuel Ugarte

Hatima ya McTominay imekuwa kwenye mashaka makubwa kwa kipindi chote hiki cha usajili, wakati klabu za Fulham na Napoli zikitajwa kuhitaji huduma yake. Man United iligomea ofa ya Pauni 20 milioni kutoka kwa Fulham mapema kwenye dirisha hili na kinachoelezwa miamba hiyo ya Craven Cottage haijakata tamaa ya kunasa saini yake. Napoli nao wanamhitaji, lakini wakimtaka kwa mkopo wa makubaliano ya kumnunua jumla kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwakani.

McTominay amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa, lakini Man United ina nguvu ya kumwongezea mwaka mmoja zaidi. Staa huyo, aliyeibukia kwenye akademia ya timu hiyo, amecheza zaidi ya mechi 250 tangu alipopandishwa kikosi cha kwanza, Aprili 2017.

Msimu uliopita alifanya vyema zaidi, akifunga mabao 10, huku akihusika kwenye mabao ya ushindi dhidi ya Brentford, Chelsea na Aston Villa kwenye Ligi Kuu England. Lakini, sasa McTominay atapigwa bei ili ipatikane za kumsajili Erik ten Hag kuboresha kikosi chake.

Man United imeonyesha dhamira ya kutaka saini ya kiungo wa PSG, Ugarte. Mchezaji huyo yupo tayari kwenda kukipiga Old Trafford, lakini shida ipo kwa klabu yake kutaka dau kubwa. PSG ipo tayari kuachana na kiungo huyo, lakini hawataki kumuuza kwa ada isiyofika Pauni 52 milioni, ambazo wao walilipa huko Sporting Lisborn ya Ureno kunasa saini yake, Julai mwaka jana.

Ugarte alicheza mechi 37 na miamba hiyo ya Ufaransa msimu uliopita, wakati PSG iliposhinda Ligue 1 na Coupe de France.