Curacao taifa dogo, kocha mzee Kombe la Dunia 2026
Muktasari:
- Kushinda au kupoteza, “Blue Wave” wapo hapa kuonyesha ubunifu wao wa kipekee na wenye rangi nyingi. Mmoja wa wachezaji wao amesema wazi kuwa wapo hapa kuchukua kombe.
WILLEMSTAD, CURACAO: CURACAO ni hadithi ya kishujaa kwenye Kombe la Dunia. Nchi ndogo ya kisiwa cha Karibiani, yenye idadi ya watu takriban 158,000 tu lakini maisha ya usiku yanayoshindana na London au New York, ipo siku nne tu kabla ya kuandika historia kama timu ndogo zaidi kuwahi kushiriki mashindano haya.
Kushinda au kupoteza, “Blue Wave” wapo hapa kuonyesha ubunifu wao wa kipekee na wenye rangi nyingi. Mmoja wa wachezaji wao amesema wazi kuwa wapo hapa kuchukua kombe.
Kikosi chao, ambacho kinajumuisha wachezaji wengi waliyozaliwa Uholanzi kimekuwa kikifundisha kucheza soka wakiwa pekupeku kwenye fukwe za nyumbani, hatua chache kutoka kwenye viti vya kupumzika vya jua na mabanda ya mbao kando ya pwani. Aina yao ya kucheza ni kama Brazil, push-up kwenye mchanga, huku wakitabasamu na kicheko kikijaza hewa yenye chumvi hewani.
Inasikitisha kiasi kwamba wapo hapa. Mwishoni mwa wiki, waliwavutia wengi baada ya kusafiri kwa basi la shule lililozeeka, wakiwa wamepanda gari ambalo halina vioo na wakionekana wakiwa wamevaa jezi zilizochoka sana. Jumapili hii wanakutana na mabingwa, Ujerumani, kwenye Uwanja wa Houston wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 72,000, sawa na karibu nusu ya idadi ya watu wa kisiwa chao, wengi watasubiri kwa hamu kubwa kuona mchezo huu wa kuvutia.
Mashabiki 5,000 pekee ndiyo wanasafiri kuishangilia timu hiyo huko Amerika Kaskazini, huku maelfu wakiwa nyumbani wakiwa mbele ya skrini katika sherehe mbalimbali kisiwa chote, kilichoko kilomita 40 kutoka pwani ya Venezuela, wakiiunga mkono timu yao, jiulize kama mashabiki 50,000 wangesema wanaondoka nchini kwenda kwenye fainali hizo maisha nchini kwao yangakuwaje? nasfikiri baadhi ya ofisini za umma zingefungwa.
“Kisiwa kitafungwa wakati michezo inaendelea,” amesema shabiki mmoja, Brenton Balentien.
“Kwetu soka ni maisha. Sisi ni kisiwa kidogo, kila mtu hapa ni familia, kufanikisha kitu kikubwa kama kufuzu Kombe la Dunia, ni jambo kubwa sana. Mbali na kuona kuzaliwa kwa watoto wangu, hili ndilo jambo bora zaidi lililotokea kwangu.”
Hii ni timu ambayo haijasahau mizizi yake. Wakati wa maandalizi yao, wachezaji wamekuwa wakishirikiana na mashabiki, kuchukua picha za pamoja, kukutana uso kwa uso, na kusaini jezi na mipira. Kuna hisia kisiwa chote kwamba wachezaji hao kwa namna fulani wako karibu sana na wananchi kwa njia ambayo mataifa makubwa hayawezi kufanikisha.
Wanaingia kwenye fainali hizi wakiwa na matumaini makubwa. Katika kampeni ya kufuzu, Curacao haikuonyesha udhaifu katika mechi zao 10, ikishinda dhidi ya Haiti, Jamaica na Trinidad na Tobago. Hii inawapa uhakika kwamba wanaweza kushindana angalau katika mashindano haya, ingawa kundi lao ni gumu haswa wakiwa na Ujerumani, Ivory Coast na Ecuador lakini bado wanaamini wanatoboa.
Kushinda dhidi ya Jamaica hakukuwa rahisi. Curacao walicheza ugenini na kuleta mashabiki wao makini kwenye ndege mbili ili kuipa hamasa timu yao katika uwanja wenye viti 35,000 mjini Kingston, lakini sehemu kubwa ya umati ilikuwa nyuma ya timu ya McClaren. Hata hivyo, wageni hao waliokuwa na rangi ya bluu waliwatawanya na hakika timu yao ikapata ilichokuwa inataka.
“Nadhani Mungu alikuwa nasi usiku huo,” amesemaLeandro Bacuna, nahodha wa Curacao.
“Kwa sababu umeona mchezo, kila mtu ameona. Mipira kadhaa uligonga kwenye, kila sehemu. Lakini kipa wetu alikuwa bora, kwa hivyo nadhani ilikuwa imetolewa kwetu. Hii ilikuwa hadithi iliyokuwa imeandikwa kwa ajili yetu.”
Mtu aliyesimamia safari ya kuanzia kwa Curacao ni kocha Dick Advocaat, raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 78, ambaye atakuwa meneja mzee zaidi kuwahi kusimamia kwenye Kombe la Dunia.
Advocaat, aliyewahi kuifundisha Sunderland alikataa nafasi hiyo Februari ili kukaa na binti yake aliyekuwa mgonjwa na kuchukuliwa nafasi na Fred Rutten, lakini alirudi Mei 2026. Kuhakikisha anaweka rekodi kwenye michuano hii.
Kisiwa hiki hakikuwa na timu ya taifa hadi 2010, walijumuishwa chini ya bendera ya Netherlands Antilles iliyofutwa kwa hivyo ni mafanikio makubwa kufika katika jukwaa la dunia miaka 16 tu mbele.
Timu yao haina wachezaji staa wengi. Jina linalojulikana zaidi ni Leandro Bacuna, aliyecheza Aston Villa kwa miaka mitatu, lakini kampeni hii inahusu zaidi jitihada ya pamoja.
Curacao ni timu ya tatu yenye kiwango cha chini zaidi kwenye mashindano haya, ikiwa nafasi ya 82 kwenye orodha ya FIFA. Ni New Zealand na Haiti pekee zenye kiwango cha chini zaidi. Lakini kwa kuwa walikuwa nafasi ya 150 miaka kumi iliyopita, wamenyanyua viwango vyao.
Kipengele muhimu, kujiamini kunaendelea kuwa ndani yao kwamba wanaweza kuleta mshtuko. Kulia-mbele Livano Comenencia, anayefanya kazi yake Zurich, Uswisi, amesemakwa FIFA:
“Tumelelewa tukicheza kwa mtindo wa Kiholanzi na tuna ujuzi halisi na mbinu bora. Tutawashangaza wengi.
“Mchezo unapoanza, chochote kinaweza kutokea. Daima ni 11 dhidi ya 11, si 5 dhidi ya 11. Kila kitu kinawezekana, hata dhidi ya Ujerumani. Nadhani alama nne zitatosha kutupeleka hatua inayofuata ya mashindano, ushindi na sare. Tutafanya kila tuwezalo kufanikisha hilo.”
“Kwa sisi, kufuzu Kombe la Dunia tayari ni hatua kubwa, kwa sababu hatujawahi kufanikisha kitu cha kiwango hiki hapo awali na tutakuwa nchi ndogo zaidi katika historia ya mashindano.
“Watu wengi tayari wanatuona kama washindi. Lakini tuna akili ya kushinda na hatuko hapa tu kuhesabiwa. Tunaenda Kombe la Dunia kwa nia ya kulishinda.”