Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cristiano Ronaldo, nahodha mwenye namba zake mbele ya Bruno

MANCHESTER, ENGLAND. CRISTIANO Ronaldo (CR7) na Bruno Fernandes ni mastaa wa soka, mashujaa wa Ureno na nyota waliocheza pamoja Manchester United, walipokutana kwa muda mfupi wakati Ronaldo aliporejea kwa Mashetani Wekundu 2021, kabla ya mgogoro wake mbaya na klabu hiyo kusababisha kuondoka kwake mwishoni mwa 2022.

Kipindi hicho kiliwaona nyota hao wawili wakicheza pamoja mara 51, huku wakiongeza mechi nyingine 67 pamoja katika timu ya taifa ya Ureno kipindi hicho hicho.

Fernandes bado yupo Old Trafford kama nahodha, huku Ronaldo akiendelea kuishi maisha ya kifahari Saudi Arabia akiwa na Al-Nassr.

Na ingawa Ronaldo ni jina kubwa zaidi kwa mbali na mmoja wa watu maarufu duniani zaidi ya kuwa mchezaji wa soka, Fernandes sasa vizuri pia hasa kutokana na mafanikio uwanjani ndani ya United alikochangia mabao 21 huku akifunga tisa katika mechi 35 alizocheza msimu ulioisha pekee.

Na moja ya asisti zake za mabao kwa Benjamin Sesko dhidi ya Everton kabla ya mechi nne za mwisho za msimu ilimfanya kufikisha mchango wa mabao 140 katika Ligi Kuu England sawa na Ronaldo. Na, labda kwa kushangaza alifanya hivyo katika michezo 10 michache zaidi, na  ameshamzidi nahodha wake wa timu ya taifa. Lakini nani ni gwiji mkubwa zaidi wa United kati yao? Daily Mail Sport inaangalia kwa karibu zaidi.


TAKWIMU ZA MOTO

Kazi za Ronaldo zimejengwa juu ya uwezo wake wa ajabu wa kufunga mabao, na anaifuata rekodi ya mabao 1,000 katika maisha yake ya soka akiwa na miaka 41. Akiianza kazi yake kama kiungo wa kulia, alikuwa mshambuliaji kamili na hajawahi kuangalia nyuma tangu hapo.

Mchezaji pekee aliyefunga mabao 100 akiwa na klabu nne tofauti sasa ana mabao 973, huku ikitarajiwa atafikia 1,000 msimu ujao kama kila kitu kitakwenda sawa. Alifunga mabao 450 katika mechi 438 akiwa Real Madrid, ambapo alicheza soka bora zaidi. Vipindi vyake viwili England vilizaa mabao 145, huku kukaa kwake muda mfupi Juventus kulimfanya afunge mara 101.

Ukijumlisha na mabao 125 akiwa Al-Nassr, matano Sporting Lisbon na 143 kwa Ureno akiwa mfungaji bora wa kimataifa wa muda wote wa nchi hiyo unapata rekodi ya kusisimua. Kwa uwiano, ni mabao 0.74 kwa kila mchezo.

Kwa upande wa Fernandes, kufunga mabao siyo jambo lake kubwa. Na, ingawa ni mdogo kwa miaka 10 kwa Ronaldo hawezi na hataweza  kufikia hata nusu ya idadi ya Ronaldo. Amefunga mabao 217 katika maisha yake hadi sasa, huku 106 kati ya hayo yakiwa kwa klabu yake ya sasa. Mabao 63 yalikuja akiwa Sporting, 11 Udinese, matano Sampdoria na manne Novara, huku akiwa amefunga 28 kwa timu ya taifa. Hiyo ni sawa na mabao 0.3 kwa kila mchezo. Hata hivyo, pasi za mabao ndizo nguvu yake kubwa. Fernandes ametoa pasi za mabao 205 katika maisha yake hadi sasa, ikiwa ni pamoja na 106 kwa United na 50 kwa Sporting. Hiyo ni wastani wa 0.28 kwa kila mchezo. Ronaldo ana asisti 307 kwa jumla, ikiwa ni pamoja na 131 kwa Real Madrid na 50 kwa United, lakini hiyo ni wastani wa 0.23 kwa kila mchezo.


MAKOMBE WALIYOBEBA

Idadi ya makombe ya Fernandes siyo kubwa. Amekuwa na United tangu 2020, na miaka yake sita Old Trafford imekuja katika nyakati ngumu zaidi katika historia ya klabu. Hata hivyo, ameshinda FA moja na Carabao moja, pamoja na tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka msimu wa 19/20 na uliopita. Lakini ukimlinganisha na Ronaldo ni mbingu na dunia, kwani miaka 10 Real Madrid ameshinda Ligi ya Mabingwa mara nne na moja akiwa United na bingwa Hispania mara mbili; Italia mara mbili; Super Cup mara mbili; Kombe la Dunia la Klabu mara nne; Kombe la FA Hispania mara mbili, Kombe la FA Italia mara moja na FA England mara moja. Pia bingwa wa EPL mara tatu, tuzo zake binafsi hazihesabiki. Hata hivyo, zinapambwa na Ballon d’Or tano. Tofauti yao kubwa sana.


UTAJIRI SASA

Ronaldo ni mmoja wa watu tajiri zaidi duniani, si tu kwa upande wa soka. Mwaka 2025, alikuwa mchezaji wa kwanza wa soka kuwa bilionea, na inakadiriwa ana utajiri wa takribani Pauni 1.04 bilioni.

Fedha hizo zimetokana na mshahara wake mkubwa inaosemekana anapata takribani Pauni 488,000 kwa wiki akiwa Al-Nassr sambamba na  udhamini, na matangazo mbalimbali. Ukweli ni kwamba ni nyota mkubwa na mashine ya kutengeneza pesa.

Miradi mingine ni pamoja na mkataba wa maisha na Nike, pamoja na kufanya kazi na kampuni kama Altice, Herbalife, DAZN. Pia ana himaya yake ya biashara. Chapa ya CR7 imemwezesha kufungua hoteli, vituo vya mazoezi, manukato na nguo za ndani  na huenda bado hajaishia hapo huku akikaribia kustaafu. Fernandes, kwa upande mwingine, anaishi maisha yanayolenga zaidi soka. Inasemekana analipwa takribani Pauni 280,000 kwa wiki akiwa United, baada ya kukataa kujiunga na Ronaldo Saudi kwa Pauni 700,000 kwa wiki huko Al-Hilal.

Wadhamini wake pia ni pamoja na Nike, huku akifanya kazi na kampuni kama Gillette na DHL. Hii inamfanya kuwa na utajiri wa takribani Pauni  78 milioni. Nje ya uwanja, Ronaldo ana maisha yake tofauti kabisa ya kifahari tofauti na Bruno ambaye bado anajikusanya.