Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cooper Flagg na Wenzake Watikisa Raundi ya Kwanza NBA Draft 2025

Muktasari:

  • Kivipi? Ni tukio ambalo linaweza kugeuza maisha ya kijana kutoka kuwa mwanafunzi wa chuo hadi nyota wa kimataifa wa kikapu ndani ya sekunde chache. Ni kipindi ambacho historia huandikwa upya.

TEXAS, MAREKANI: KATIKA kila kona ya Marekani kipindi cha “NBA Draft” kinatazamwa kwa jicho la matumaini, hofu na msisimko.

Kivipi? Ni tukio ambalo linaweza kugeuza maisha ya kijana kutoka kuwa mwanafunzi wa chuo hadi nyota wa kimataifa wa kikapu ndani ya sekunde chache. Ni kipindi ambacho historia huandikwa upya.

Kama ulikuwa hufahamu, NBA Draft ni tukio la kila mwaka ambalo hufanyika chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Marekani (NBA), likiwa na lengo la kuruhusu timu zote za NBA kuchagua wachezaji wapya  hasa kutoka vyuoni, shuleni au nje ya Marekani. Mwaka huu, Cooper Flagg ameingia kwenye vitabu vya rekodi akiwa chaguo la kwanza la NBA Draft akichaguliwa na timu ya Dallas Mavericks.

Kwa mvuto wa hadithi yake na kipaji kilichojidhihirisha mapema, Flagg amejiunga na orodha ya wachezaji waliowahi kuwa namba moja akifuata nyayo za watu kama LeBron James (2003), Shaquille O’Neal (1992), na Allen Iverson (1996).


FLAGG NA WENZAKE

Flagg ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakisubiriwa kwa hamu. Akiwa na urefu wa futi 6.7 na uwezo wa kucheza mbele. Flagg pia ni mlinzi makini na mfungaji mahiri. Akiwa chuoni Duke alikuwa na wastani wa alama 19.7 kwa mchezo pamoja na ribaundi 8.5 huku akizuia mashambulizi wastani wa 2.8.

Nyota mwingine ni Dylan Harper mwenye damu ya kikapu kwani baba yake ni nyota wa zamani wa NBA, Ron Harper. Akitokea Chuo cha Rutgers, Harper ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kuongoza mchezo.

Ana urefu wa futi 6.4 na uwezo wa kucheza kama ‘point guard’ana takwimu za alama 18.2, asisti za mwisho 7.3 na kuiba mipira 2.1 kwa kila mchezo. Harper anajiunga na Spurs ambako atacheza na Victor Wembanyama.

Valdez Drexel Edgecombe ni mchezaji kutoka Bahamas aliyejifunza kikapu Marekani. Akiwa Baylor, Edgecombe alijizolea sifa kwa ufungaji kutoka maeneo mbalimbali ya uwanja akiwa na wastani wa alama 20.5, ribaundi 6.1 na mafanikio ya asilimia 41 katika mitupo ya mbali. Sasa anakwenda kujiunga na Philadelphia 76ers na matarajio ni kwamba atapunguza mzigo kwa Joel Embiid.

Kon Knueppel ni mmoja wa watupiaji bora zaidi wa kizazi hiki.

Akiwa na urefu wa futi 6.4 na uwezo wa kucheza katika nafasi tatu aling’ara akiwa Duke. Kwa Hornets, ambayo muda mrefu imekuwa ikihitaji mchezaji wa kuaminika katika nafasi ya pembeni ujio wake unaweza kuwa suluhisho.

Ace Bailey, sawa na Dylan Harper anatokea Chuo cha Rutgers na amekuwa mmoja wa wachezaji waliovutia zaidi kwa uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali kutokana na urefu na wepesi. Akiwa na urefu wa futi 6.8, Bailey ni mchezaji anayefaa kwenye mfumo wa kisasa wa kikapu ambapo nafasi si kikwazo. Alifunga wastani wa alama 21.1, ribaundi 7.9 na kuzuia 1.5 kwa kila mchezo.

New Jazz wanamchukulia kama jiwe la msingi kwenye ujenzi mpya wa timu na huenda akawa mmoja wa nyota wakubwa wa ligi ndani ya miaka michache ijayo.

Kwa ujumla wachezaji hao  wameonyesha viwango vya juu walipokuwa vyuoni na sasa wanachukuliwa kama nyota wapya wa kesho.

Ikiwa wataendelezwa vizuri na kupewa nafasi katika vikosi, NBA inaweza kushuhudia kizazi kingine cha wachezaji wenye ushawishi mkubwa wakibeba matumaini ya timu na mashabiki.


NINI KILITOKEA

Mabadiliko ya karne ya 21 yameifanya NBA Draft kuwa tukio la kimataifa. Hali hiyo imejidhihirisha kwa uteuzi wa nyota kutoka kila kona ya dunia. Mwaka 2023, Victor Wembanyama kutoka Ufaransa alichaguliwa na San Antonio Spurs.

Mwaka mmoja kabla Paolo Banchero mwenye asili ya Italia alichaguliwa na Orlando Magic.