Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern, Barca ni jino kwa jino kwa Dusan Vlahovic

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Barca inatafuta mshambuliaji ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski ambaye anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

BARCELONA inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Serbia, Dusan Vlahovic, mwenye umri wa miaka 25, ambaye anatarajiwa kuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu.

Barca inatafuta mshambuliaji ambaye anaweza kuchukua nafasi ya Robert Lewandowski ambaye anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Bayern Munich pia imetajwa kuwa na nia ya kumsajili Vlahovic, kwa sababu haina uhakika wa kuendelea kuwa na Harry Kane, 32, kwa muda mrefu kutokana na kipengele kilichopo katika mkataba wake ambacho kinamruhusu kuondoka mwisho wa msimu ikiwa timu inayomhitaji italipa kiasi kinachofikia Pauni 55 milioni.

Vilevile, Bayern inaona umri wa Kane ni mkubwa hivyo, inahitaji mchezaji itakayekuwa naye kwa muda mrefu zaidi na Dusan ndio anaonekana kuivutia zaidi.


Bruno Fernandes

MANCHESTER United inadaiwa kuhitaji ada ya takribani Pauni 40 milioni ili kumruhusu kaptemi wao raia wa Ureno, Bruno Fernandes, 31, kuondoka katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

 Staa huyu anahitajika sana na Bayern Munich na baadhi ya timu za Saudi Arabia ambazo zipo tayari kumpa mshahara mnono ili akibali kutua katika timu zao. Bruno, ambaye amechezea Man United kwa misimu kadhaa, amekuwa mhimili wa timu hiyo licha ya kuhusishwa kuondoka.


Nico Williams

LIVERPOOL inapanga kuwasilisha ofa ya takribani Euro 90 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Athletic Club, Nico Williams, mwenye umri wa miaka 23. Nico ameng’ara sana La Liga kwa misimu kadhaa pamoja na timu ya taifa hususani mwaka jana ambapo aliisaidia Hispania kushinda taji la Euro. Timu kibao ikiwamo Barcelona zilihitaji kumsajili katika dirisha lililopita lakini ilishindikana.


Nico Schlotterbeck

LIVERPOOL inataka kuwasilisha ombi kwa Borussia Dortmund ili kumsajili beki wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Schlotterbeck ana uwezo wa kucheza kama beki wa kati au kushoto jambo ambalo litakuwa ni suluhisho la suala la majeruhi kwa Liverpool.


Elliot Anderson

KIUNGO wa kati wa Nottingham Forest, Elliot Anderson, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 22, yupo kwenye orodha ndefu ya wachezaji wanaowindwa na Newcastle United kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

 Newcastle imepanga kutoa zaidi ya Pauni 40 milioni ili kumrudisha mchezaji huyo ambaye alicheza katika akademi yao akiwa mdogo.


Upamecano

REAL Madrid inafuatilia kwa karibu ishu ya beki wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, Dayot Upamecano, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyu anadaiwa kutohitaji kuendelea kusalia Bayern na yupo tayari kusikiliza ofa kutoka sehemu nyingine ili kupata changamoto mpya. Madrid inaripotiwa kumshawishi asikubali kusaini mkataba na badala yake ajiunge nao akiwa mchezaji huru.


Endrick

TAARIFA za ndani kutoka Real Madrid zinadai kuwa timu hiyo ina mpango wa kumtoa mshambuliaji wake chipukizi Endrick kwa mkopo wa nusu msimu katika dirisha lijalo la usajili wa Januari ili apate muda mwingi zaidi wa kucheza. Hata hivyo, West Ham United ambayo inahusishwa naye sio kati ya machaguo yanayopewa kipaumbele na mchezaji pamoja na Madrid yenyewe.


Nathaniel Brown

ARSENAL ndio inaonekana kiwa kinara katika vita ya kuiwania saini ya  beki kisiki wa Eitranch Frankfurt na timu ya taifa ya Ujerumani, Nathaniel Brown, 22. Hata hivyo, licha ya uwepo wa vigogo wengi ikiwamo Manchester City na Real Madrid, wanaohitaji huduma ya staa huyu, Frankfurt  imepanga kutopokea ofa yoyote hadi itakapofika mwisho wa msimu huu.

Nathaniel Brown ni miongoni mwa mastaa walioonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha Frankfurt tangu ajiunge nacho.