Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca yaamua jambo kwa Lewandowski, Milan yatajwa

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao, alijiunga na Barca  mwaka 2022 akitokea Bayern Munich na tangu wakati huo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kwanza cha wababe hao wa Nou Camp.

BARCELONA haina mpango wa kumsainisha mkataba mpya  mshambuliaji wake wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 37 ambaye anawindwa na AC Milan.

Staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao, alijiunga na Barca  mwaka 2022 akitokea Bayern Munich na tangu wakati huo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha kwanza cha wababe hao wa Nou Camp.

Barca inataka kuachana na Lewandowski ili kupunguza bili ya mshahara na kuweza kuingiza majina ya wachezaji wapya itakaowasajili mwakani.

Miongoni mwa wachezaji wanaodaiwa kusababisha fundi huyu asipewe mkataba mpya ni pamoja na Marcus Rashford ambaye Barca inataka kumsainisha mkataba wa kudumu katika dirisha la majira ya joto mwakani.


Jordan Pickford

KIPA wa Everton na timu ya taifa ya England, Jordan Pickford, mwenye umri wa miaka 31, yupo mbioni kusaini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu yake.

Pickford, ambaye ameichezea Everton tangu mwaka 2017 baada ya kusajiliwa kutoka Sunderland, amekuwa nguzo muhimu kwa Everton na timu ya taifa ya England ambako kote amekuwa chaguo la kwanza.

Mkataba wa sasa wa Pickford unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


William Osula

NEWCASTLE United inafikiria kumruhusu mshambuliaji wao wa kimataifa wa Denmark, William Osula, 22, kuondoka kwa mkopo katika dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kuwasilisha ombi la kutaka kuruhusiwa.

Hata hivyo, kabla ya kumruhusu, Newcastle inataka kuhakikisha wachezaji wengine wote wa safu ya ushambuliaji hawana majeraha yoyote. Osula anataka kuondoka Newcastle kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza.


Lucien Agoume

ARSENAL inamtazama kiungo wa kati wa Sevilla, Lucien Agoume, 23, kama mmoja kati ya wachezaji ambao inataka kuwasajili  katika dirisha la usajili la Januari.

Agoume ambaye ni raia wa Ufaransa, ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha Sevilla na anadaiwa kumvutia sana kocha Mikel Arteta ambaye alitamani kuipata huduma yake tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Mkataba wa sasa wa Agoume unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Ronald Araujo

CHELSEA inaonyesha nia ya kumsajili beki wa kati wa Barcelona, Ronald Araujo mwenye umri wa miaka, 26, lakini kuna uwezekano mdogo wa uhamisho huo kufanyika Januari. Araujo ambaye ni tegemeo katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya Uruguay, anaweza akauzwa kwa zaidi ya Pauni 60 milioni. Mkataba wa Araujo unatarajiwa kumalizika mwaka 2031. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 7 michuano yote.


Richarlison

ORLANDO City SC bado inapambana kuhakikisha inaipata saini ya  mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Richarlison, 28, katika dirisha kubwa la usajili wa majira ya kiangazi mwakani.

Inaelezwa Orlando tayari imeanza mazungumzo ya awali na wawakilishi wa Richarlison kuhusu uwezekano wa uhamisho huo, ambao utakuwa sehemu ya maboresho yanayoendelea katika kikosi chao.

Richarlison, ambaye kwa sasa ana mkataba na Spurs hadi 2027, ameichezea timu ya taifa ya Brazil mechi 52 na kufunga mabao 21.


Axel Disasi

BORUSSIA Dortmund inataka kumsajili beki wa Chelsea, ambaye kocha Enzo Maresca ametoa ruhusa ya kuuzwa au kutolewa kwa mkopo katika dirisha lijalo. Inaelezwa Maresca amekataa kumjumuisha Disasi katika kikosi chake licha ya klabu hiyo kukumbwa na tatizo la majeraha. Inaelezwa Maresca anaona Disasi haendani na mifumo yake na aliruhusu auzwe.


Nico Schlotterbeck

BARCELONA imeanza mazungumzo na Borussia Dortmund kwa ajili ya  kumsajili beki wa klabu hiyo na timu ya taifa ya Ujerumani, Nico Schlotterbeck, mwenye umri wa miaka 25, ambaye atakuwa huru mwisho wa msimu huu. Schlotterbeck ni miongoni mwa mabeki bora wa Ujerumani katika miaka ya hivi karibuni na Barca inamwona kama chaguo sahihi lisilo na gharama.