Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca ijayo... Harry Kane, Rashford chama Moja

RASHFORD (1)

Muktasari:

Klabu hiyo ya Catulanya imemweka Kane kuwa chaguo la kwanza kwenye mpango wao wa kumtafuta mrithi wa Robert Lewandowski, ambaye mkataba wake utafika ukomo mwakani.

BARCELONA, HISPANIA: HABARI ndo hiyo. Barcelona inafanya mpango wa kuhakikisha masupastaa wa England, Harry Kane na Marcus Rashford wanacheza pamoja kwenye fowadi yao msimu ujao.

Klabu hiyo ya Catulanya imemweka Kane kuwa chaguo la kwanza kwenye mpango wao wa kumtafuta mrithi wa Robert Lewandowski, ambaye mkataba wake utafika ukomo mwakani.

Mabingwa hao wa La Liga bado hawajafikia makubaliano ya mkataba mpya na supastaa wa Poland, Lewandowski na inaweza kurudi tena Bayern Munich kwenda kunasa saini ya straika mwingine veterani.

Kitu kizuri ni kwamba Kane anaweza kupatikana kama tu atapenda kuhama kutokana na kipengele kilichowekwa kwenye mkataba wake huko Allianz Arena.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur, ambaye amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 kwenye klabu moja iliyopo kwenye Ligi Kuu tano bora za Ulaya, alisajiliwa na Bayern Munich kwa ada ya Pauni 86.4 milioni mwaka 2023.

RASH 01

Lakini, mabingwa hao wa soka wa Bundesliga watalazimika kumruhusu mshambuliaji huyo aondoke endapo kama itawekwa mezani ofa ya Pauni 57 milioni tu kwenye dirisha la majira ya kiangazi mwakani. Mkataba wa Kane huko Bayern Munich utafika tamati 2027, lakini wanakabiliwa na ulazima wa kumruhusu kuondoka kama atasakwa na timu mpya kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya baridi, Januari.

Barcelona inamtazama Kane, 32, kama mbadala sahihi wa mshambuliaji Lewandowski, huku wakifurahishwa na kiwango chake cha uwanjani akifunga mabao 23 katika mechi 17 alizocheza msimu huu, huku Bayern ikifurahia mwanzo mzuri kwenye Bundesliga.

Uhamisho wa Kane utamfanya kuwa staa wa pili wa kimataifa wa England kwenda kucheza Catalunya, huku Rashford akifanya vyema kwa mkopo katika kikosi cha Barcelona akitokea Manchester United. Barca inaweza kuufanya uhamisho wa Rashford kuwa wa moja kwa moja katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick amekuwa akivutiwa na kiwango cha Rashford hadi sasa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 yupo tayari kubaki Nou Camp.

RASH 02
RASH 02

Lakini, Kane bado kutakuwa na nguvu kubwa kumshawishi akubali kuhama. Akizungumza mwezi uliopita, straika huyo alikiri kwamba akili yake kwa sasa ameielekeza kwenye kuichezea Bayern na amekuwa na mpango wa kurudi kwenye Ligi Kuu England.

"Katika ishu ya kubaki muda mrefu, hilo ni suala la kusubiri na kuona," amesema.

"Sijawahi kuwa na mazungumzo na Bayern, lakini kama wataamka na kutaka kuzungumza nitakuwa tayari kwa hilo," amesema.

Lakini, kama Barca itatimiza ndoto ya kumsajili Kane na kisha ikafanikiwa kubaki na huduma ya Rashford kwa msimu ujao, basi wakali hao wa kimataifa wa England, watakwenda kuongoza safu ya ushambuliaji ya miamba hiyo ya Nou Camp sambamba na Lamine Yamal.