Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aston Villa yampa masharti mazito Marcus Rashford

TETESI Pict

Muktasari:

  • Rashford kwa sasa ni mmoja kati ya wachezaji wanaokunja pesa nyingi zaidi katika Ligi Kuu England akilipwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki kiasi ambacho Aston Villa imemwambia kuwa haiwezi kumlipa.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 27, ameambiwa kuwa akubali kupunguza mshahara wake ikiwa anataka kusaini mkataba wa kudumu wa kuendelea kuitumikia Aston Villa aliyojiunga nayo kwa mkopo katika dirisha lililopita la majira ya baridi, Januari, mwaka huu.

Rashford kwa sasa ni mmoja kati ya wachezaji wanaokunja pesa nyingi zaidi katika Ligi Kuu England akilipwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki kiasi ambacho Aston Villa imemwambia kuwa haiwezi kumlipa.

Tangu alipojiunga na timu hiyo yenye maskani yake jijini Birmingham, Rashford ameonekana kuwa katika kiwango bora akicheza mechi 11 ambapo ameifungia mabao matatu na kutoa asisti nne.

Mkataba wake wa sasa na Man United unatarajiwa kumalizika 2028.


Nico Williams

ARSENAL imeambiwa kwamba itatakiwa kumlipa winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams, 22, mshahara utakaomfanya kuwa mmoja kati ya mastaa wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi katika kikosi ikiwa inataka kuipata huduma yake. Nico ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027, msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kufunga mabao tisa.


Lorenzo Lucca

MANCHESTER United imemuweka katika orodha ya juu mshambuliaji wa Udinese, Lorenzo Lucca, 24, kwenye listi ya mastaa ambao inataka kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Italia, amelivutia benchi la ufundi la Manchester United kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika kikosi chake huko Italia tangu kuanza kwa msimu huu.


Dejan Kulusevski

TOTTENHAM Hotspur inapambana kuhakikisha inambakisha kiungo raia wa Sweden, Dejan Kulusevski, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, ambapo timu vigogo kibao zimeonyesha nia ya kumsajili ikiwa ni pamoja na AC Milan na Napoli. Kocha wa Spurs, Ange Postecoglu bado ana mipango na Dejan na hataki kuona akiondoka. Mkataba wake unamalizika 2028.


Stefan Ortega

BAYER Leverkusen imewasiliana na wawakilishi wa kipa wa Manchester City na timu ya taifa ya Ujerumani, Stefan Ortega, 32, ambaye inaweza kusajiliwa kwa ada ya uhamisho ya Euro 8 milioni. Ortega ni miongoni mwa wachezaji ambao hawapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha Pep Guardiola na mkataba wake unamalizika 2026.


Kobbie Mainoo

KIUNGO wa Manchester United, Kobbie Mainoo amewaambia wawakilishi wake kwamba lengo la kwanza ni kusaini mkataba mpya kuendelea kusalia kwa Mashetani Wekundu licha ya utitiri wa timu zinazotaka kumsajili katika dirisja lijalo. Mainoo mwenye umri wa miaka 19, saini yake inawindwa na Inter Milan, Chelsea na Real Madrid. Mkataba wake unamalizika 2027.


Arda Guler

WINGA wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uturuki, Arda Guler amefanya makubaliano binafsi na Aston Villa ili kujiunga nayo katika dirisha la majira ya kiangazi kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja. Guler mwenye umri wa miaka 20, amekuwa hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Madrid jambo linalomfanya ahitaji kuondoka.


Oleksandr Zinchenko

ARSENAL inataka kufanya maboresho katika kikosi chake kwa msimu ujao ambapo inataka kuwaondoa wachezaji wasiopungua 11 ili kusajili wengine. Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na beki wa kushoto raia wa Ukraine, Oleksandr Zinchenko mwenye umri wa miaka 28 na beki kisiki wa timu taifa ya Poland, Jakub Kiwior, mwenye umri wa miaka 25.