Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ashangaa shabiki kumtunza fedha kwa ushindi US Open

US Pict

Muktasari:

  • Paolini alipata ushindi mwepesi dhidi ya Mtaliano mwenzake Lucrezia Stefanini akimshinda kwa seti mbili za 6-4, 6-1 katika mchezo uliochezwa asubuhi kwenye uwanja wa nje.

NEW YORK, MAREKANI: KUONA mashabiki Tanzania wakimtunza fedha mchezaji akiwafurahisha uwanjani si habari, lakini Marekani imekuwa tukio kubwa baada ya shabiki mmoja kumpa zawadi ya fedha mcheza tenisi kwenye mashindano ya US Open.

Hiyo ilitokea jana wakati nyota wa tenisi wa Italia, Jasmine Paolini amepewa zawadi ya aina yake baada ya ushindi wake kwenye Uwanja wa 5 katika michuano ya US Open inayoendelea.

Paolini alipata ushindi mwepesi dhidi ya Mtaliano mwenzake Lucrezia Stefanini akimshinda kwa seti mbili za 6-4, 6-1 katika mchezo uliochezwa asubuhi kwenye uwanja wa nje.

Baada ya mchezo huo, Paolini alikuwa akisaini autografu na kuwasalimia mashabiki alipokutana na mwanamke mmoja mwenye nywele za njano aliyekuwa amevaa miwani ya jua.

Mwanamke huyo alitoa noti ya dola mbilina kumpa Paolini. Awali, Paolini alidhani shabiki huyo alitaka amtie saini noti hiyo, lakini mwanamke huyo akamwambia:

“Ni yako. Ni noti ya dola mbili, ni nadra kuonekana na inawakilisha bahati nzuri.”

Paolini alimshukuru shabiki huyo, ambaye pia alimshauri kuihifadhi noti hiyo kwenye begi lake kwa muda wote wa mashindano.

Inaonekana noti hiyo ilikuwa na ujumbe fulani wa kumtakia Paolini, ambaye ni mchezaji namba 19 kwenye michuano ya wanawake, bahati njema. Paolini aliishikilia mbele ya kamera huku akionekana kushangazwa na zawadi hiyo.

USA 01

SI NADRA SANA, LAKINI...

Ingawa noti ya dola mbili si adimu kihalisi, takribani noti bilioni 1.7 za aina hiyo bado zinatumika nchini Marekani, si noti inayopatikana mara kwa mara ikilinganishwa na jumla ya takribani noti bilioni 55.6 za karatasi zinazozunguka nchini humo.

Akizungumza na New York Post, Paolini amesema nilifikiri ilikuwa zawadi nzuri. Aliniambia hii ndiyo ya bahati. Akaniambia, ‘ihifadhi kwa ajili yako.’ Nikasema sawa, nikaiweka kwenye begi na itabaki nami. Tutaona kama itafanya kazi. Hilo ndilo muhimu.”

USA 02

PAOLINI AENDELEA NA SAFARI

Paolini alifunga ushindi huo kwa urahisi katika seti ya pili baada ya seti ya kwanza kuwa na ushindani mkali. Alishinda seti ya kwanza 6-4 baada ya Stefanini kurudisha mpira wa huduma yake na kuutumbukiza kwenye nyavu. Paolini, anayeshika nafasi ya 21 duniani, hajawahi kufika zaidi ya hatua ya 16 bora katika US Open, mafanikio aliyoyapata mwaka 2024.

Mwaka huo pia alifikia fainali za Roland Garros na Wimbledon, hivyo mashabiki wa Italia wanatumaini noti hiyo ya dola mbili itamletea “bahati” ya kwenda mbali zaidi safari hii.

Baada ya kutinga raundi ya tatu, Paolini sasa anakabiliwa na Sorana Cîrstea wa Romania, anayeshika nafasi ya 16 katika michuano hiyo.