Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marefa wetu FIFA muongeze umakini

MAREFA Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa watu muhimu ambao hawatakiwi kuichezea nafasi hii tamu ya kunufaika na AFCON 2027 ni marefa wetu wa hizi nchi tatu hasa Tanzania.

KUNA kama muda wa miezi nane umebaki kabla ya kufanyika kwa fainali za AFCON 2027 ambazo Tanzania tutaziandaa kwa pamoja na Kenya na Uganda.

Haya ni mashindano ambayo yanapaswa kutunufaisha sisi waandaaji nje na ndani ya uwanja maana mcheza kwao hutuzwa na sio yawe na faida kubwa kwa wageni.

Hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anatakiwa ajipange hasa kuhakikisha anatumia vizuri fursa ya uwepo wa mashindano hayo makubwa zaidi Afrika.

Miongoni mwa watu muhimu ambao hawatakiwi kuichezea nafasi hii tamu ya kunufaika na AFCON 2027 ni marefa wetu wa hizi nchi tatu hasa Tanzania.

Bongo hapa marefa wetu wamekuwa na bahati mbaya ya kukosa fursa ya kuchezesha mashindano makubwa kama hayo yanayokuja au yale ya Kombe la Dunia.

Sasa AFCON inachezwa kwetu hivyo ni wazi marefa wetu watapewa kipaumbele cha kuchezesha lakini kabla ya hilo kutimia ni lazima wao wenyewe wadhihirishe kama wanastahili.

Kuanzia sasa, marefa wetu tunaowategemea ambao ni wale wenye beji za FIFA, wanatakiwa kujilinda kwa kuhakikisha wanachezesha vizuri mechi mbalimbali watakazopangiwa.

Kijiwe kinaamini kwamba kwa kufanya hivyo, hao wanaowateua watashawishika na kuona haja ya kuwapa nafasi kwenye hayo mashindano yanayokuja.

Kinyume na hapo, watawapa ugumu mabosi zao na wataishia kuona wenzao wa nje wakipewa filimbi za kuchezesha AFCON huku wao wakibaki kuwatazama japo mashindano yanachezwa nyumbani.