Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Asafiri km 11,987 kumwona staa wa Brazil

SAFARI Pict

Muktasari:

  • Brazil ilianza vizuri kwenye mashindano hayo huku Clarinha akiwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa kikosi hicho kinachosubiri kuandika historia mpya.

INAELEZWA binamu wa nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Ana Clara Oliveira 'Clarinha' alisafiri kilomita 11,987 kutoka Brazil hadi Poland kwa ajili ya kumshuhudia ndugu yake akicheza na kufunga bao kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea Poland.

Brazil ilianza vizuri kwenye mashindano hayo huku Clarinha akiwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa kikosi hicho kinachosubiri kuandika historia mpya.

Safari ya binamu huyo kwa ndugu yake mchezaji haikuwa rahisi kwani inaelezwa aliondoka Goiânia, akapitia Brasília, São Paulo, Berlin na Kraków kabla ya kufika Bielsko-Biala, huku safari yote ikimchukua zaidi ya saa 24.

SAFA 01

André anatumia kiti cha magurudumu baada ya kupata ajali mwaka 1997 akiwa na miaka 16, lakini hilo halikumzuia kutimiza ahadi yake.

Amesema alimuahidi Clarinha kama angefika Kombe la Dunia, angekuja kumwona Poland. “Nilikuwa mtu pekee niliyekuja hapa kutoka Brazil, nikiwa kwenye kiti cha magurudumu, nikikabiliana na safari ya ndege ya saa 11 kutoka São Paulo hadi Ujerumani, kisha nikasafiri kwa saa kadhaa zaidi hadi Poland,” amesema Andre.

Akizungumzia hilo nyota huyo amesema “Huyu ni godfather wangu, André kuwa kwake hapa kuna maana kubwa sana kwangu.”

SAFA 02

“Ajali ilitokea kabla hajazaliwa, kwa hiyo hivyo ndivyo alivyonifahamu. Hivyo ndivyo nilivyo kama godfather wake, Kwa Clarinha, hilo halijawahi kuwa jambo la kumfanya ajisikie tofauti au kuwa kikwazo. Uhusiano tulionao ni kama vile tumefahamiana tangu maisha mengine na yeye ni mtu wa kipekee sana.”