Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nahodha KMKM amtaja Fiston Mayele

NAHODHA Pict

Muktasari:

  • Kauli ya Charles imekuja baada ya Mayele kufunga bao la pili katika ushindi wa mabao 3-0 ilioupata Al Ahli Tripoli dhidi ya KMKM, mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyochezwa Septemba 5, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

NAHODHA msaidizi wa KMKM, Martin Charles, amesema licha ya mshambuliaji wa Al Ahli Tripoli, Fiston Mayele kutupia bao kwenye mechi yao ya kwanza, lakini haikuwa kazi ngumu kumdhibiti.

Kauli ya Charles imekuja baada ya Mayele kufunga bao la pili katika ushindi wa mabao 3-0 ilioupata Al Ahli Tripoli dhidi ya KMKM, mechi ya raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyochezwa Septemba 5, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Charles amesema, haikuwa kazi ngumu kumkabili Mayele ambaye ni moja ya washambuliaji hatari kwa sababu walifanya kwa kushirikiana na wenzake.

Alieleza kuwa, kama wangeshindwa kufanya hivyo maana yake Mayele angefanikiwa kufunga mabao mengi zaidi.

“Haikuwa kazi ngumu kwetu kumdhibiti Mayele kwani hilo tulilifanya kwa umoja ndio sababu ya kushindwa kufunga mabao mengi,” amesema Charles.

Amesema wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano nchini Libya na watahakikisha wanawafunga wapinzani wao. Charles amesema, makosa waliyoyafanya mechi ya kwanza ndio yamewagharimu akikiri kwamba mawasiliano kati ya kipa na mabeki yalikosekana.

Alibainisha kwamba, wamerudi uwanja wa mazoezi kusawazisha makosa hayo ili kuhakikisha wanarudi na ushindi kuanzia mabao manne, matokeo wanayotakiwa kuyapata ili wavuke.

Ikumbukwe kuwa, kabla ya mchezo huo, Charles amesema Mayele hawezi kuwa tishio kwao kwa sababu uwanjani hachezi peke yake, hivyo walijiandaa kumzuia na kubakisha ushindi nyumbani.