Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta atangaza jeshi lake Ligi ya Mabingwa Ulaya

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Mbrazili huyo bado hajapona vyema majeraha yake baada ya kuumia goti Januari mwaka huu wakati Arsenal ilipopoteza dhidi ya Manchester United kwenye Kombe la FA.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amempiga chini Gabriel Jesus kwenye kikosi cha timu yake kitakachoshiriki mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika hatua ya ligi msimu huu.

Mbrazili huyo bado hajapona vyema majeraha yake baada ya kuumia goti Januari mwaka huu wakati Arsenal ilipopoteza dhidi ya Manchester United kwenye Kombe la FA.

Arteta ametaja kikosi cha mastaa 23 kutoka kwenye Orodha A huku idadi kamili ya wachezaji wote wanaopaswa kushiriki michuano hiyo kwa kila timu ni 25.

Wachezaji walioibukia kutoka kwenye akademia kama Ethan Nwaneri na Myles Lewis-Skelly, wao wanakidhi kutajwa kwenye Orodha B kwa sababu walizaliwa 2004 kupanda juu, lakini kipa Max Dowman, ambaye alifikisha miaka 15, Desemba mwaka jana, ameorodheshwa kwenye Orodha A.

ARS 01

Kwenye Orodha A ya wachezaji 23 inajumuisha wachezaji wanane wapya waliosajiliwa dirisha hili la majira ya kiangazi: Kepa Arrizabalaga, Piero Hincapie, Cristhian Mosquera, Martin Zubimendi, Christian Norgaard, Noni Madueke, Ebere Eze na Viktor Gyokeres. Kuna nafasi ya kipa kinda Tommy Setford, aliyejiunga na Arsenal akitokea Ajax mwaka 2024.

Kama Arsenal itapenya na kufikia kwenye hatua ya mtoano, itakuwa na nafasi ya kuongeza watu kwenye kikosi chao. Dowman atahamishiwa kwenye Orodha B atakapotimiza umri wa miaka 16, hapo atatoa nafasi kwenye Orodha A ili Jesus aingie endapo kama atakuwa fiti kurudi kikosini.

Kutokana na hilo, Dowman atakuwa kwenye nafasi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya endapo kama atapewa nafasi ya kucheza kabla ya kufika mwakani. Rekodi hiyo kwa sasa inashika na mkali wa Borussia Dortmund, Youssoufa Moukoko, ambaye alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 18 wakati alipoitumikia klabu yake hiyo ya Ujerumani dhidi ya Zenit St Petersburg mwaka 2020.

ARS 02

Kinda mwenye kipaji maridhawa kabisa Dowman tayari ameshaweka rekodi ya kuwa kinda wa pili kuwahi kucheza kwenye Ligi Kuu England, sambamba na Nwaneri. Atafikisha umri wa miaka 16 Mwaka Mpya, hivyo dakika moja tu endapo kama atapangwa na Arsenal kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya atavunja rekodi ya Moukoko.

Arsenal itaanza kampeni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ugenini dhidi ya Athletic Bilbao, Septemba 16, wakati mechi ya pili itakayocheza nyumbani itapigwa siku 15 baadaye dhidi ya Olympiacos. Kisha itakipiga dhidi ya Atletico Madrid, Slavia Prague, Bayern Munich na Club Brugge kabla mwaka kumalizika na baada ya hapo itakipiga na Inter Milan na Kairat Almaty, Januari mwakani. Msimu uliopita, Arsenal ilimaliza namba tatu kwenye hatua ya ligi, huku kwenye mechi nane ilizocheza hatua hiyo, ilipoteza dhidi ya Inter Milan tu.

Hatua ya mtoano ilizisukuma nje PSV Eindhoven na Real Madrid kabla ya kukwama mbele ya Paris Saint-Germain kwenye hatua ya nusu fainali.

Kikosi cha Arsenal cha Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/26.

Makipa: David Raya, Kepa Arrizabalaga, Tommy Setford.

Mabeki: William Saliba, Cristian Mosquera, Ben White, Piero Hincapie, Gabriel, Jurrien Timber, Riccardo Calafiori.

Viungo: Martin Odegaard, Eberechi Eze, Christian Norgaard, Leandro Trossard, Noni Madueke, Mikel Merino, Kai Havertz, Martin Zubimendi, Declan Rice, Max Dowman.

Washambuliaji: Bukayo Saka, Gabriel Martinelli, Viktor Gyokeres.