Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yakomaa kwa Viktor Gyokeres, Atletico yajitosa

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mbali na Arsenal na baadhi ya timu za England kumhitaji, ripoti zinaeleza Atletico Madrid pia inahitaji huduma ya fundi huyu na imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake.

ARSENAL inajiandaa kurejea na ofa nyingine kwa mshambuliaji wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Sweden, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 27, dirisha lijalo.

Mbali na Arsenal na baadhi ya timu za England kumhitaji, ripoti zinaeleza Atletico Madrid pia inahitaji huduma ya fundi huyu na imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake.

Hivi karibuni ripoti zilieleza Gyokeres ambaye msimu uliopita alicheza mechi 52 za michuano yote na kufunga mabao 54  msimu uliopita, ameonyesha nia zaidi ya kujiunga na Arsenal.

Mkataba wa sasa wa straika huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Sporting ipo tayari kumwachia fundi huyu lakini kwa timu itakayokuwa tayari kulipa Euro 100 milioni ambayo ipo katika mkataba wake.

Man United pia inapambana kuinasa saini yake licha ya kuonekana kupungua kasi.


Antoine Semenyo

MANCHESTER United inataka kumgeukia mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa itashindwa kuipata saini ya staa wa Brentford na timu ya taifa ya Cameroon, Bryan Mbeumo. Mbali ya Semenyo, Man United pia imepanga kumsajili kiungo wa kati wa Crystal Palace na England, Eberechi Eze, mwenye umri wa miaka 26.


Mathys Tel

TOTTENHAM Hotspur inataka kumsainisha mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Bayern Munich, Mathys Tel, 20, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, baada ya kuvutiwa na kiwango kikubwa alichoonyesha msimu uliopita alipokuwa akicheza kwa mkopo katika kikosi chao. Tel ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu uliomalizika alicheza mechi 34 za michuano yote na inaonekana hana mpango wa kurudi Bayern.


Javi Guerra

AC Milan imewasiliana na Valencia kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 22, Javi Guerra katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Guerra ni mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Valencia na msimu uliopita alicheza mechi 38 za michuano yote na kuwavutia Milan ambayo inataka kuimarisha kikosi chake kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia.


Hakan Calhanoglu

INTER Milan iko tayari kusikiliza ofa kutoka kwa timu zinazohitaji huduma ya kiungo wao wa kimataifa wa Uturuki, Hakan Calhanoglu, mwenye umri wa miaka 31. Staa huyu inadaiwa kuwa katika rada za Galatasaray ambayo inataka kumsajili dirisha lijalo. Mkataba wa kiungo huyu unamalizika mwaka 2027. Inter inataka kuuza baadhi ya nyota wake na kusajili wapya watakaorudisha makali msimu ujao kuwania mataji.


Justin Kluivert

BAYER Leverkusen imewasiliana na Bournemouth kuulizia uwezekano wa kuipata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo na timu ya taifa ya Uholanzi, Justin Kluivert, kama mbadala baada ya kiungo wao raia wa Ujerumani, Florian Wirtz, mwenye miaka 22, kutakiwa na Liverpool. Kluivert ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Bournemouth na kiwango chake kimeivutia Leverkusen.


Adama Bojang

WEST Ham imefanya mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa Reims na timu ya taifa ya Gambia, Adama Bojang, 21, kuhusu uwezekano wa kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Bojang ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika  mwaka 2028,msimu uliopita alicheza mechi 27 za michuano yote.


Adrien Truffert

MABOSI wa Bournemouth wamefanya makubaliano na Rennes kuhusu kumsajili beki Adrien Truffert, mwenye miaka 23, ambaye inamchukua kama mbadala wa beki wao wa kushoto wa kimataifa wa Hungary, Milos Kerkez, mwenye umri wa miaka 21, anayetarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Liverpool katika dirisha lijalo.