Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, Brighton, Man City wang'ara, Spurs shaka

ZANG'ARA Pict

Muktasari:

  • Ingawa msimu bado una safari ndefu, baadhi ya timu zimeonyesha kiwango cha kuvutia, huku nyingine zikikabiliwa na changamoto na kuanza kwa kusuasua.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England imesimama kwa muda wa wiki tatu kutokana na mapumziko ya kimataifa, huku mechi za ligi zikitarajiwa kurejea Oktoba 10, baada ya timu kucheza michezo mitano ya mwanzo wa msimu.

Ingawa msimu bado una safari ndefu, baadhi ya timu zimeonyesha kiwango cha kuvutia, huku nyingine zikikabiliwa na changamoto na kuanza kwa kusuasua.

Hivi ndivyo tathmini ya BBC ilivyozipa timu hizo baada ya michezo mitano ya ligi:


Arsenal – Alama 7

Arsenal imeanza vizuri katika kutetea taji lake, lakini ilikumbana na kipigo kizito kutoka kwa Brighton baada ya kunusurika kupigiwa penalti dhidi ya Sunderland.


Aston Villa – Alama 6

Kuna dalili za kuanza kurejea katika mwelekeo mzuri baada ya kupoteza wachezaji kadhaa muhimu katika dirisha la usajili.


ZANG 02

Bournemouth – Alama 6

Kama mechi zingemalizika dakika ya 80, Bournemouth ingekuwa miongoni mwa timu za juu kwenye msimamo. Hata hivyo, inahitaji kuacha tabia ya kufungwa mabao katika dakika za mwisho.


Brentford – Alama 8

Imeonyesha kiwango bora katika mwanzo wake wa msimu bila kupoteza, ikizifumua Tottenham na Chelsea. Swali ni kama itaendeleza kiwango hicho na kupigania nafasi ya kushiriki mashindano ya Ulaya.


Brighton – Alama 9

Brighton imekuwa miongoni mwa timu zinazotoa burudani zaidi, ikiwa imefunga mabao 16 katika mechi tano za ligi, ikiwamo matatu dhidi ya mabingwa Arsenal. Ni timu inayofurahisha kuitazama.


Chelsea – Alama 6

Baada ya kuanza vizuri chini ya kocha Xabi Alonso, Chelsea imepoteza mechi mbili kati ya tatu zilizopita na kufichua udhaifu wake katika mchezo dhidi ya Brentford. Hali hiyo imeibua maswali kuhusu mwelekeo wa timu hiyo.


Coventry City – Alama 6

Ushindi dhidi ya Nottingham Forest Jumamosi uliwapa nafuu kubwa, huku mashabiki wa Coventry wakionekana kuondokana na presha. Sasa macho yanaelekezwa kuona kama kikosi cha Frank Lampard kitaendeleza matokeo hayo.


Crystal Palace – Alama 5

Bado ina nafasi kubwa ya kuboresha kiwango chake baada ya kushinda mechi moja na kupoteza tatu.


Everton – Alama 6

Licha ya kupitia dirisha la usajili lisilokuwa la kuridhisha, kocha David Moyes ameifanya Everton kuwa timu ngumu kushindwa.


ZANG 01

Fulham – Alama 5

Fulham imepata sare nzuri dhidi ya Liverpool na Manchester United, lakini inahitaji ushindi. Mechi dhidi ya Ipswich ugenini, Hull City nyumbani, Coventry ugenini na Crystal Palace nyumbani zinaweza kuipa matumaini baada ya mapumziko ya kimataifa.


Hull City – Alama 8

Kufikisha pointi nane katika mechi tano za mwanzo zenye ushindani mkubwa ni matokeo mazuri. Hull imeifunga Manchester United na kupata sare dhidi ya Aston Villa na Chelsea.


Ipswich Town – Alama 5

Licha ya kuonyesha udhaifu katika ulinzi, ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Sunderland na Crystal Palace umeiwezesha kupata pointi sita, huku ikionyesha moyo wa kupambana.


Leeds United – Alama 7

Ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo, Leeds bado haijapoteza na ina rekodi bora ya ulinzi inayolingana na timu nyingine. Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle umeonyesha uwezo wake.

ZANG 04

Liverpool – Alama 6

Liverpool bado haijapoteza, lakini haijaonyesha kiwango chake bora. Haijaruhusu bao katika mechi tatu zilizopita, ingawa inatarajiwa kufanya zaidi.


Manchester City – Alama 9

Mechi tano za ligi, ushindi mara tano. Manchester City iliishinda Manchester United licha ya kubaki na wachezaji 10 baada ya mchezaji mmoja kutolewa katika kipindi cha kwanza. Erling Haaland akiwa tayari anaongoza kwa ufungaji mabao, mashabiki wa City wanatarajia timu hiyo kupigania ubingwa.


Manchester United – Alama 4

United imeonyesha kiwango cha kukatisha tamaa baada ya kupoteza dhidi ya Hull na kutoka sare na Fulham, iliyokuwa mkiani mwa msimamo. Ushindi wake pekee ulipatikana dhidi ya Ipswich, huku sare ya dakika za mwisho dhidi ya Everton ikiinyima pointi tatu.


Newcastle United – Alama 6

Chini ya kocha mpya Matthias Jaissle, Newcastle imeonyesha viwango vinavyotofautiana. Iliwavutia mashabiki kwa sare dhidi ya Liverpool na ushindi mzuri dhidi ya Tottenham, lakini ilicheza vibaya katika kipigo cha Leeds kabla ya kurejea na kuifunga Hull.

ZANG 03

Nottingham Forest – Alama 5

Matokeo yake bora yamepatikana ugenini, ikiwamo sare dhidi ya Liverpool na ushindi dhidi ya Aston Villa. Hata hivyo, kiwango chake nyumbani ni chanzo cha wasiwasi, kwani haijafunga bao katika mechi tatu za City Ground na imekusanya pointi moja pekee.

Sunderland – Alama 5

Baada ya kumaliza nafasi ya saba msimu wa 2025/26, mashabiki wa Sunderland walitarajia mwanzo bora zaidi. Timu hiyo ilionyesha ushindani dhidi ya Arsenal na Manchester City, lakini ilipoteza mechi zote mbili.


Tottenham Hotspur – Alama 2

Baada ya kutumia zaidi ya pauni milioni 300 katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, Tottenham imeanza vibaya, ikishindwa kufunga bao katika mechi zake nne za mwanzo za ligi. Mashabiki wanatarajia mabadiliko ya haraka baada ya mapumziko ya kimataifa.