Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Andre Onana ageukia tiba ya moto

ONANA Pict

Muktasari:

  • Onana, mwenye umri wa miaka 30, ambaye bado ni mchezaji wa Manchester United lakini yuko kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki, ameonyesha mbinu ya tiba inayohusisha matumizi ya vikombe maalumu pamoja na moto.

LONDON, ENGLAND: KIPA wa zamani wa Manchester United, Andre Onana, ameibua gumzo baada ya kuonekana akitumia njia isiyo ya kawaida katika jitihada za kurejesha kiwango chake.

Onana, mwenye umri wa miaka 30, ambaye bado ni mchezaji wa Manchester United lakini yuko kwa mkopo katika klabu ya Trabzonspor ya Uturuki, ameonyesha mbinu ya tiba inayohusisha matumizi ya vikombe maalumu pamoja na moto.

Tiba hiyo, inayojulikana kama cupping therapy, hutumia vikombe vinavyowekwa kwenye ngozi na kutengeneza msukumo wa kuvuta ngozi, kwa lengo la kusaidia kupunguza mkazo wa misuli na kuchochea mzunguko wa damu baada ya mazoezi au shughuli za mwili.

Hata hivyo, matumizi ya moto katika mchakato huo si jambo la kawaida, lakini Onana ameonekana kulikumbatia akiamini linaweza kumsaidia kurejea katika kiwango bora wakati wa mapumziko ya kimataifa.

ONA 01

Kipa huyo wa Cameroon yuko katika harakati za kujenga upya maisha yake ya soka nchini Uturuki baada ya kipindi kigumu akiwa Manchester United, klabu aliyojiunga nayo mwaka 2023.

Baada ya kufanya makosa kadhaa yaliyomfanya apoteze nafasi yake katika kikosi cha kwanza, hatimaye alipelekwa kwa mkopo Trabzonspor.

Inadaiwa pia Manchester United bado inalipa mshahara wake licha ya kuwa kwa mkopo, huku kukiwa na matarajio kwamba anaweza kuondoka kabisa klabuni hapo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi au baada ya kumalizika kwa mkataba wake mwaka 2028.

ONA 03

Kwa upande wa Trabzonspor, msimu umeanza kwa matokeo mchanganyiko. Timu hiyo ilitolewa kwenye mchujo wa Europa League kabla ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa mabao 2-1 dhidi ya Amed SK.

Hata hivyo, walirejea kwa nguvu na kuichapa Genclerbirligi mabao 5-0 katika mchezo uliofuata, huku Onana akipata clean sheet yake ya kwanza msimu huu.

Baada ya michezo sita, Trabzonspor ilikuwa katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi.

Kabla ya mapumziko ya kimataifa, Trabzonspor ilipata ushindi mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Galatasaray, ingawa Onana hakuitwa katika kikosi cha Cameroon kwa michezo ya kimataifa.

ONA 02

Jambo jingine lililomvutia Onana ni urafiki wake usiotarajiwa na nyota wa zamani wa Liverpool, Mohamed Salah, ambaye alijiunga na Trabzonspor baada ya kuondoka Anfield na kufunga hat-trick katika ushindi huo wa mwisho wa wiki.

Sasa, Onana anaonekana kutumia kila njia inayowezekana kurejesha makali yake, huku tiba hiyo ya moto ikiwa miongoni mwa mbinu zake mpya za kujiandaa kwa safari yake ya kurejea kileleni.